Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Nazareth Tample la Ipagala, Dodoma, Askofu Dk. Evance Chande (kushoto) akimkabidhi kitabu alichokitunga cha Kutimia kwa Mpango wa Mungu Kupitia Mateso Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde wakati wa hafla ya kuzindua kitabu hicho na kutoa shukrani za kumaliza ujenzi wa kanisa hilo Novemba 22, 2020. Mavunde alinunua kitabu hicho kwa sh. 500,000.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mgeni rasmi John Malasa akizindua kitabu cha Kutimia kwa Mpango wa Mungu kupitia Mateso kilichotungwa na Askofu Dk. Evance Chande. Pamoja na mambo mengine kitabu hicho kinaelezea umuhimu kuendelea wa kudumisha amani nchini.Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Nazareth Tample la Ipagala, Dodoma, Askofu Dk. Evance Chande (kushoto) akimkabidhi Diwani wa Kata ya Ipagala , Dotto Gombo kitabu alichokitunga cha Kutimia kwa Mpango wa Mungu Kupitia Mateso wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho na kutoa shukrani za kumaliza ujenzi wa kanisa hilo Novemba 22, 2020. Pia kilizinduliwa kitabu cha aina hiyo kilichotafsiriwa kwa lugha ya kiingereza.
Askofu Dk Chande na Dotto Gombo wakiwa na furahaMgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi huo, John Malasa akimpongenza Mtunzi wa kitabu hicho, Askofu Dk. Chande kwa kazi kubwa aliyoifanya ya utunzi pamoja na kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Asanterabi Sangendi akiangalia kitabu baada ya kukinunua.
Profesa Emmanuel Shija Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Los Angels Marekani akielezea jinsi watakavyosaidia kuendeleza kipaji cha utunzi wa vitabu cha Askofu Chande.
Sehemu ya waumini wa kanisa hilo waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu na kutoa shukrani kumalizika kwa ujenzi wa kanisa hilo.
Kwaya ikitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
Muonekano wa kanisa hilo
Post a Comment