Mufti wa Tanzania Abubakari Zuberi (katikati) akimkabidhi funguo Sheikh wa Msikiti wa Masjidi Suleiman nuur, sheikh nasoor wakati wa uzinduzi uliofanyika katika msikiti huo Kinondoni Dar es Salaam, ambao umefadhiliwa na Taasisi ya Kijamii ya Alfidaus ambayo msikiti umegharimu Sh. mil 185. Kushoto kwa mufti ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Alfidaus Seleh Alhinai, kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa. PICHA NA ASHRACK MIRAJI
Mufti Abubakari Zuberi akipeana mkono na mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Masijd Suleiman nuur sheikh Salim Ahmed wakati akiwasili kwenye msikiti huo
Mufti amewashukuru Sana Tasisi ya Alfidaus na kuwataka wawe na moyo huo kujitolea pia waangalie sehemu mbalimbali za watanzania wenye uhitaji waweze kuwasaidia Mungu atawalipa Zaidi/
Mufti wa Tanzania, Abubakari Zuberi akiwa anasoma dua kwenye jengo hilo lenye gorofa sita Kinondoni linalojengwa na Taasisi ya Alfidaus iliopo hapa nchini. Kushoto ni Katibu Mkuu Bakwata, Hassan Chizega na kulia ni Katibu wa Alfidaus, Saleh Alhnai .
Post a Comment