Featured

    Featured Posts

NMB YAFUNGA MWEZI WA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUWANOA WATOTO


Meneja wa NMB Tawi la Oyster Plaza –  Hildegard Mung’ong’o akiangalia jinsi mtoto Myreen Rashid akiweka pesa ikiwa ni sehemu ya kujifunza kuhusu kuweka tangu wakiwa watoto. 

 

Watoto wakiwa katika Tawi la Benki ya NMB Oyster Plaza wakipata elimu ya fedha.

…………………………………………………………………………………….

 Katika kuhitimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja, Benki ya NMB, imewakutanisha na kuwapa watoto zaidi ya 25 elimu kuhusu masuala ya kuweka akiba na nidhamu ya fedha.

Akizungumza wakati wa utoaji elimu huo, ulioambatana na ufunguaji wa akaunti mbalimbali zilizo chini ya mwamvuli wa WAJIBU, Meneja wa NMB Tawi la Oyster Plaza – Hildegard Mung’ong’o, alisema elimu waliyopewa watoto hao ililenga kuwajengea utamaduni endelevu wa kuweka akiba tangu wakiwa wadogo.

Hildergard alibainisha kuwa, Tawi lake pamoja na matawi yote ya NMB nchini huwa yanajisikia Furaha kukutana na watoto pamoja na wazazi kuwapa elimu juu ya masuala ya kifedha (WAJIBU)  inayojumuisha akaunti tatu za Mtoto Akaunti, Chipukizi Akaunti na Mwanachuo Akaunti.

Kwa upande wake, Meneja Miradi wa Masula ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), Lilian Kisamba, alisema WAJIBU ni mwamvuli chanya katika ukuaji wa mtoto kielimu na kinidhamu ya fedha, ulioanza tangu mwaka 2016.Tangu hapo, WAJIBU kupitia akaunti za Mtoto, Chipukizi na Mwanachuo, umeweza kuwafikia zaidi ya watoto 90,000 kote nchini.  

Mameneja hao waliwataka wazazi na walezi kujitokeza matawini kufungua akaunti za watoto ambazo licha ya kadi ya Benki kuwa nayo mtoto, mzazi atabaki kuwa msimamizi mkuu wa akaunti kwa kutambua miamala inayofanyika.

NMB kupitia WAJIBU, imelenga kuwa na taifa la kesho lenye uelewa wa kina wa elimu ya masuala ya fedha, ndio maana ikaanzisha mpango maalumu unaowajumuisha mzazi na mtoto, wakiamini wateja hujengwa tangu wakiwa wadogo.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana