Featured

    Featured Posts

RAIS WA BURUNDI AMPONGEZA DK MAGUFULI KWA USHINDI MNONO

 


Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amempongeza Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli,  baada ya hapo jana kutangazwa rasmi kuwa ndiye mshindi wa kiti hicho baada ya kupata kura  12,516,252.

Rais Ndayishimiye ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo pamoja na pongezi hizo, amewapongeza pia Watanzania kwa kuiamua kesho yao ya amani na kwamba wameonesha ukomavu wa demokrasia.

“Kwa niaba ya watu wa Burundi, na kwa niaba yangu mwenyewe, ninatoa pongezi zangu za dhati kwa Rais Magufuli kwa kuchaguliwa tena, ninawapongeza pia Watanzania ambao wameamua maisha yao ya baadaye kwa amani na kuonesha ukomavu wao wa kidemokrasia” Rais Ndayishimiye
e

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana