**************************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo ameshiriki hafla ya Mwaka Mpya wa Kihindu ambapo ametoa wito kwa Wahindi na wananchi kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Katika Muhula wa pili wa uongozi ili aweze kutimiza yote aliyoahidi.
Aidha RC Kunenge ametoa Rai kwa wananchi wa Mkoa huo kulipa Kodi ili kuiwezesha Serikali kutoa huduma Bora kwa Wananchi.
Katika mahadhimisho hayo yaliyofanyika Jijini Dar es salaam, RC Kunenge amewataka Wahindi kuchangamkia fursa zote zinazopatikana nchini na kuhakikisha wanazingatia sheria.
Pamoja na hayo RC Kunenge amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inasimamia suala la Amani na Utulivu Jijini humo ili kila mmoja aweze kufanya Shughuli zake kwa usalama.
Post a Comment