Baadhi ya viongozi wa upinzani nchini, wanashikiliwa na polisi baada ya kutangaza kupanga maandamano amani siku ya leo Jumatatu kwa madai ya kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi Mkuu.
Polisi wanasema wamemkamata mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Chadema, Freeman Mbowe pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Boniface Jacob.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema walipiga marufuku maandamano hayo yaliyopangwa kuanza leo asubuhi, lakini viongozi wa Chadema "wameonekana kufanya vikao kuratibu maandamano ya fujo".
Amesema viongozi hayo walipanga kuhatarisha usalama wa raia kwa kufanya vurugu kuonesha kutokubaliana na matokeo, watu hao wanapanga kuingia mtaani kuchoma maeneo mbalimbali kama masoko, magari na vituo vya mafuta.
Aidha amesisitiza kuwa operesheni kubwa inaendelea kwa yeyote ambaye atashiriki kuratibu, kuwezesha au kushiriki katika maandamano hayo atafikishwa kwenye mikono ya sheria.
Post a Comment