Wakala Pini Zahavi imemtoa kama ofa mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Bayern Munich David Alaba kwa Real Madrid lakini Juventus na Inter Milan pia zinapenda kumnasa mchezaji huyo, 28 raia wa Austria, ambaye mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu. (Calciomercato - in Italian)
AC Milan imemfanya mlinzi wa Barcelona, Emerson, 21 ambaye anacheza kwa mkopo katika klabu ya Real Betis, kuwa mchezaji wanayemuhitaji zaidi msimu ujao. (Todofichajes-in Spanish)
Mshambuliaji wa Brazil hana mpango tena wakujiunga na Barcelona na mchezaji huyo, 28 anaona bora kusalia Paris St-Germain ( AS-in Spanish)
Kocha wa Napoli Gennaro Gattuso amebainisha kuwa nyota James Bond Sir Sean Connery, aliyepoteza maisha siku ya Jumamosi, alijaribu wakati mmoja kumshawishi kutoondoka Rangers. (Sky Sports)
Kocha wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri anaongoza katika orodha ya watakaochukua nafasi ya Bappe Lachini ikiwa atafukuzwa na Fiorentina. (Calciomercato)
Mshambuliaji wa Brazil, Gabriel Jesus, 23, ameonesha picha yake akiwa mazoezini na kikosi cha Manchester City. (Manchester Evening News)
Wolves wana mpango wa kumnyakua beki wa kulia wa Middlesbrough Djed Spence,20, wakati wa dirisha la usajili la mwezi Januari. (Teamtalk via Birmingham Mail)
Post a Comment