Featured

    Featured Posts

DK TULIA AHIRIKI USAFI KWENYE MIFEREJI JIJINI MBEYA

 

December 18, 2020 Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika Dr. Tulia Ackson ameungana na Wananchi wa maeneo mbalimbali kwa lengo la kufanya usafi katika mfereji wa maji wa Ilolo unaokusanya maji kutoka katika kata saba za Jiji la Mbeya.

“Siku ya Jumatatu nilikuja kukagua hii mifereji baada ya kuelezwa kuhusu changamoto wanazopitia Wananchi kwa hii mifereji pindi inapoziba na kusababisha maji kuingia kwenye nyumba za watu na nikapendekeza itapofika siku ya leo wote tuungane kwa lengo la kufanya usafi kila eneo la mifereji na niwashukuru sana kwa muitikio wenu mkubwa”-Dr. Tulia Ackson

“Naamini zoezi hili likiwa endelevu itatusaidia kupunguza kasi ya mafuriko ambayo yamekuwa yakitukumba mara kwa mara hususani katika vipindi vya mvua ambayo zaidi yamekuwa yakitokana na kuzibwa kwa hii mifereji, tujitahidi pia kuwa wasafi na tuache tabia za kutupa takataka katika mitaro”-Dr. Tulia Ackson

    


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana