Featured

    Featured Posts

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU DESEMBA 14, 2020

 

Sami Khedira
Maelezo ya picha,

Sami Khedira athibitisha kuzungumza na Everton

Kiungo wa kati wa Juventus Mjerumani Sami Khedira, 33, ambaye anapanga kuhama klabu hiyo mwezi Januari, amethibitisha kuwasiliana na mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti. (Bild - in German)

Everton wako tayari kumpatia ofa ya uhamisho wa bila malipo kiongo wao wa kati Dele Alli, 24 mwezi Januari kwa lengo la kuikosesha Tottenham Hotspur nafasi ya kumsajili. (Star)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema kuwa kiongo wa kati Mhispania Isco hayuko katika mipango yake ya siku zijazo. Hata hivyo, kiungo huyo aliye na umri wa miaka 28-anatarajiwa kuondaka klabu hiyo mwezi Januari. (Marca - in Spanish)

Isco

Mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon, 31, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Dalian Pro, China amehusishwa na tetesi za kuhamia Wolves kushikilia nafasi ya Raul Jimenez aliyejeruhiwa. (Sun)

Paris St-Germain huenda ikamsajili mshambuliaji wa Lyon Mholanzi Memphis Depay msimu ujao lakini Barcelona wamekuwa wakimnyatia kwa muda mrefu kiongo huyo aliye na umri wa miaka 26. (Le Parisien - in French)

Tottenham wako tayari kulipa Juventus £63.6m kumunua mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27. (TodoFichajes - in Spanish)

Paulo Dybala
Maelezo ya picha,

Tottenham wako tayari kulipa Juventus £63.6m kumnunua Paulo Dybala

Kiungo wa kati wa Lyon Mfaransa Houssem Aouar, 22, ambaye amekuwa akinyatiwa kwa muda mrefu na Arsenal, pia analengwa na Paris St-Germain huku klabu hiyo ikitarajiwa kuanza mazungumzo kumhusu mchezaji huyo hivi karibuni. (RMC - in French)

Klabu za Leeds na West Ham ni miongoni mwa Ligi ya Primia ambazo zinamsaka mlinzi wa MK Dons Matthew Sorinola,(Teamtalk)

Mazungumzo ya kuandaa pigano kati ya Anthony Joshua na Tyson Fury mwaka 2021 huenda yakachukua "siku chache" kukamilishwa, promota Eddie Hearn ameesema.

Anthony Joshua v Tyson Fury

Joshua ambaye alimpiga knockout Kubrat Pulev siku ya Jumamosi imeanzisha matarajio ya mapigano kati ya wapinzani wa Uingereza.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana