Serikai ya Eswatini imesema kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ,Ambrose Dlamini amefariki dunia, wiki nne baada ya kupatikanava virusi vya corona.
Taarifa ya serikali imesema kuwa Bw Dlamini, mwenye umri wa miaka 52, alifariki dunia Jumapili mchana hospitalini nchini Afrika Kusini.
Hakuna sababu ya kifo iliyotajwa, lakini hivi karibuni Dlamini alitibiwa maradhi ya Covid-19 nchini Afrika Kusini.
Dlamini amekuwa waziri Mkuu wa Eswatini, zamani ikiitwa Swaziland, tangu mwezi wa Oktoba 2018.
Nchi hiyo ndogo iliyopo kusini mwa Afrika ni moja ya nchi chache ambazo bado zinatawaliwa kifalme duniani.
Ikiwa na idadi ya watu wapatao milioni moja tayari imerekodi visa 6,768 vya virusi vya corona na vifo127 vilivyohusishwa na corona, kwa mujibu wa Wizara ya afya.
Dlamini alitangaza kuwa amepatwa na virusi vya corona tarehe 16 Novemba. Wakati huo alisema kuwa hakuwa na dalili na anahisi vyema.
Wiki chache baadaye , tarehe 1 Disemba, serikali ya Eswatini ilisema kuwa Dlamini amehamishiwa katika hospitali ya Afrika Kusini kwa matibabu , kwa lengo la kuharakisha kupona kwake.
Lakini Jumapili serikali ilisema kuwa Dlamini amefariki "wakati alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Afrika Kusini ", bila taarifa zaidi .
"Serikali kwa ushirikiano na familia itaendelea kulifahamisha taifa kuhusu mipango kadri inavyoendelea," Naibu Waziri Mkuu Themba Masuku alisema katika taarifa
Post a Comment