Featured

    Featured Posts

BASHE AWEKA HISTORIA, AWA MBUNGE WA KWANZA KUWASILISHA MPANGO WA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM 2020-2021


Mbunge wa Nzega Hussein Bashe akizungumza wakati wa kuwasilisha Mpangokazi wake wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-25 katika Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Serene, Nzega mjini, Jumamosi, Januari 16, 2021.


Nzega, Tabora.

Mbunge wa Nzega Mjini na Naibu Waziri wa KIlimo Hussein Bashe, ameandika historia katika Siasa za Tanzania katika awamu hii ya Pili ya Uongozi wa Rais Dk. John Magufuli kwa kuwa Mbunge wa kwanza kuwasilisha Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020 - 2025, katika jimbo la lake la Nzega Mjini mkoani Tabora.


Bashe ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo wa kuchaguliwa, kwa awamu ya Pili, amedhihiri sifa yake hiyo, baada ya kuwasilisha Taarifa ya Mpango wa Utekelezaji was Ilani ya CCM kwa kipindi hicho Cha 2020-2025 katika Mkutano was Sina yake uliofanyika Jumamosi iiliyopita, ya Januari 16, 2021 katika ukumbi wa Sarene, Nzega Mjini mkoani Tabora.


Mkutano huo  uliweza kutia fora kutokana na kuhudhuliwa na viongozi was ngazi na kada kutokana Wilaya ya Nzega  wakiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, Wakuu wa Idara na watendaji mbalimbali wa Serikali, Wakuu wa shule, Taasisi za Fedha, Taasisi za Dini, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya matawi hadi Wilayani.


Mpango wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 uliowasilishwa na Mheshimiwa Bashe umegawanyika katika vipindi vya miaka mitano inayoonyesha muelekeo wa jimbo la Nzega Mjini katika kutekeleza Ilani hiyo ya CCM, ahadi za Rais Dk. Magufuli pamoja na ahadi binafsi za mbunge.


Aidha, mpango huo umeanisha vipaumbele vya kimaendeleo pamoja na miradi ya kimkakati itakayosimamiwa na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini pamoja na Halmashauri ya Mji wa Nzega ili kuchochea maendeleo ya haraka katika Mji wa Nzega.


Ili kuweza kukamilisha mpango huo jumla ya fedha za kitanzania 100,690,340,000 zinahitajika kukamilisha miradi mbalimbali ndani ya Mji wa Nzega huku serikali Kuu ikiwa ni mbia ambaye atachangia asilimia 84 ya bajeti yote, Fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri kuchangia asilimia 12 na Mbunge wa Nzega Mjini pamoja na wananchi wanatarajiwa kuchangia asilimia 4 ya fedha zote za kufanikisha mpango huu Kwa muda wa miaka mitano huku katika mwaka 2021/2022 kiasi cha shilingi bilioni 18.7 zikiwa zinahitajika katika kutekeleza miradi mbalimbali iliyoainishwa kwenye mpango huu wa Utekelezaji wa Ilani.


Miradi ya kimkakati inayotarajiwa kufanikishwa  katika kipindi cha miaka mitano kama ilivyotajwa katika mpango ni pamoja na;

1.Mradi wa ujenzi wa Stendi ya Kisasa Nzega 

2.Mradi wa ujenzi wa Soko la Kimataifa la vitunguu

3.Miradi ya skimu za umwagiliaji 

4.Ujenzi wa Shule mpya za msingi 4

5.Ujenzi wa zahanati pamoja na vituo vya afya 

6.Ujenzi wa kituo cha Taaluma nzega (Nzega Centre of Excellence)

7.Kuongeza ufadhili wa Masomo kwa wanafunzi ngazi zote 

8.Ujenzi wa barabara Kati ya Mji na miundombinu ya kuzuia mafuriko 

9.Uboreshaji wa upatikanaji wa huduma za Maji Kwa kila kaya 

10.Upatikanaji wa huduma za umeme kwenye kila kijiji na vitongoji ili kuchochea ujasiriamali na ukuaji uchumi 

11.Ujenzi wa mabweni Kwa ajili ya wanafunzi wa kike kwneye shule zote za Sekondari 


Bashe anasema “Mipango yetu ni kuufanya Mji wa Nzega kuwa mji wa hadhi ya biashara ya usafirishaji kwani ni njia panda ya kwenda maeneo mengi nchini na nchi jirani”


“Tunalenga kujenga stendi kubwa itakayokuwa pia na maeneo ya mapumziko ndani yake, vituo vya wafanyabaishara wadogo pamoja na kuweka viwanja. Hii ndio Nzega tunayotamani na kulenga kufikia; na ili kufikia ndoto hii lazima tuwe na mikakati na mipango yenye uwezo wa kutekeleza mema”


Aidha, Mheshimiwa Bashe ameeleza ya kuwa “mpango wetu ni kuhakikisha tunaondoa umasikini wa watu lakini Kwa wakati huo huo tunainua elimu ndani ya Mji wetu wa Nzega Kwa kuhakikisha watoto wote wanaotakiwa kwenda shule wanakwenda shuleni Kwa wakati”


“Kwa jamii masikini kama zetu, Elimu ndio ufunguo wa kushinda maadui wengine wote wa taifa letu. Maarifa na ujuzi unapoongezeka ndivyo watu wetu wanavyoweza kuongeza kipato chao na kushiriki Kuijenga nchi yao”


“Mpango wetu wa Utekelezaji wa Ilani umeonyesha wazi kuwa tutajikita zaidi katika sekta ya Elimu kama kipaumbele cha msingi na tutaongeza uwekezaji katika sekta hii ili kuhakiksiha elimu haiwi tu haki ya msingi ila jambo la kilazima Kwa watoto wetu wa Nzega pasipo kujali uwezo wa kaya au historia ya mtoto”


Mheshimiwa Bashe ameweka wazi dhamira yake ya kujenga soko kubwa la kimataifa la vitunguu Katika mji wa Nzega ikiwa ni sehemu ya kuchochea ukuaji wa Mji wa Nzega na kuongeza kipato cha wananchi wa Mji huo.


Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega ndugu Amos Kanuda amesema ya kwamba “Bashe ni Mbunge wa kipekee sana jambo hili linamfanya kuwa Mbunge pekee ambaye ameweza kutengeneza mpango wa kitaalamu wa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi Kwa kuangalia mazingira ya Mji wetu wa Nzega, kazi hii ni kubwa na ya kupongezwa na kuigwa na viongozi wengine kwenye maeneo mengi nchini”


Mwenyekiti Kanuda aliendelea kusema ya kuwa “wajibu wa serikali na watumishi wake ni  kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi Kwani msingi wa serikali ni watu ambao walikipa ridhaa Chama cha mapinduzi baada ya kuamini kuwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ndio Ilani bora kuliko za vyama vyote na ina uwezo wa kupatia maendeleo wanayoyahitaji”


Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega amewaagiza watendaji wote wa serikali kuhakikisha watekeleza miradi yote ya kimkakati ambayo inagusa maisha ya wananchi moja Kwa moja hasa zikiwemo barabara na ujenzi wa mifumo bora ya Maji ili kupunguza athari zitokanazo mvua zinazoendelea Kunyesha.


Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega ndugu Philemon Magesa amesema “halmashauri ya Mji imepokea maelekezo ya Chama na mapendekezo yote yaliyomo Kwenye mpango wa utekelezaji na kuwakaribisha wafanyabiashara katika mji wa Nzega kufika katika Ofisi yake Kwa haraka pale kunapokuwa na shida yeyote ili kuhakikisha kunakua na mahusiano mazuri baina ya serikali na wafanyabiashara ambao ni walipa kodi Katika halmashauri ya Mji wa Nzega”


Mwisho kabisa Mbunge wa jimbo la Tunduma na  Naibu Waziri wa Tamisemi ndugu David Silinde aliyefika ukumbini kusalimia akiwa safarini kuelekea Dodoma alisema ya kuwa “Maendeleo yeyote katika eneo lolote yanahitaji maridhiano baina ya viongozi wa Chama, serikali na utayari wa wananchi katika kushirikiana na viongozi wao”


Silinde alibainisha ya kuwa “Hakuna kiongozi ambaye hakosei lakini hatutakiwi kutegana kwenye makosa ili kuumizana tunakiwa kushirikiana na kusaidiana kwa pamoja mana sisi wote lengo letu ni kuhakikisha maeneo yetu na watu tunaowaongoza wanapiga hatua za kimaendeleo.”


Pia, Mheshimiwa Bashe amemshukuru Rais Magufuli kwa kufanikisha ujenzi wa shule mpya mbili za bweni za jinsia ya kike na jinsia ya kiume zilizoko kwenye kata ya Mwanzoli na Kitangili; ujenzi na upanuzi wa kituo cha Afya cha Zogolo pamoja na ukarabati wa miundombinu ya Maji huku fedha zote zikiwa ni fedha za nje ya bajeti zilizofanikishwa kupitia Rais Magufuli.


Mwisho, Mheshimiwa Bashe na Silinde kwa pamoja wamemshukuru Rais Magufuli na Chama cha Mapinduzi kwa Imani kubwa kwao na kuahidi kutumia uwezo wao wote katika kuhakikisha jamii masikini nchini zinapata maendeleo kupitia miradi ya kiserikali kwenye sekta wanazosimamia.

Habaripicha👇













Picha zote na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Nzega.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana