Featured

    Featured Posts

KANISA HALISI LAFANYA KWA KISHINDO IBADA MAALUM YA KUFUNGUA BIASHARA YA UTALII UKANDA WA KASKAZINI, DC ALITABIRIA KUJA KUWA KANISA KUBWA TANZANIA

 Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha Frank Mwaisumbe akizungumza kabla ya kuanza Ibada maalum ya kufungua Biashara ya Utalii Ukanda wa Kaskazini, iliyofanywa na Kanisa Halisi la Mungu Baba la Tegeta jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Mwishoni mwa wiki iliyopita. Mkuu huyo wa Wilaya alimwakilisha Mkuu wa mkoa huo Iddi Kimanta kuwa mgeni rasmi. Kulia ni Mkuu wa Kanisa hilo Baba wa Uzao akiwa na Mama wa Uzao

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu huyo wa mkoa, Mkuu huyo wa Wilaya alisema, Kwa kuamua kufanya Ibada hiyo, Kanisa Halisi la Mungu Baba limezidi kujipambanua kuwa ni Kanisa la kipekee, kwa sababu limejikita katika mahubiri na mafundisho ya kumwabudu Mungu ambayo yanaigusa jamii ya Watanzania wote.

"Mbali na hii ibada maalum mliyoandaa ya kufungua Biashara ya Utalii Ukanda wa Kaskazini, lakini mimi nimekuwa nikifuatilia mahubiri ya Kanisa hili, na nimegundua kuwa mafundisho na mahubiri yako Baba wa Uzao yamekuwa yakiigusa jamii ya Watanzania wote kwa kuwa kwa sehemu kubwa huwa yanalenga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania wote na nchi kwa jumla", alisema Mkuu huyo wa Wilaya na kuongeza; 

"Kwa hali hii naamini Kanisa Halisi litakuja kuwa Kanisa kubwa ndani na Nje ya Tanzania, Baba wa Uzao nakutakia kila la Kheri na Mungu awabariki mfike mbali".

"Sote tunatambua kuwa Rais Dk. John Magufuli ni muumini na Mchamungu wa kweli, lakini ameweza kuongoza Serikali kutokana na msaada wa uwepo wenu ninyi waumini wa dini. kwa hiyo nakupongeza sana Baba wa Uzao kwa kuamua kubeba jukumu hili, Asante sana Baba wa Uzao, asante sana waumini wote wa Kanisa Halisi", alisema Mkuu wa Wilaya na kuongeza;

"Umezungumza mambo manne yaliyokufanya uwe hapa, lakini nimeshangazwa sana kwa kuamua kubeba wajibu huu wa kuombea Utalii hasa hapa Arusha. Ni kweli kabisa wananchi wengi katika ukanda huu wanategemea sana utalii, na ugonjwa huu wa Korona ulipoingia umewaathiri sana wananchi, kwa hiyo jukumu hili ulioamua kulifanya ni la muhimu sana".

Mapema akimkaribisha kuzungumza, Baba wa Uzao alitangulia kufanya Ibada ya shukrani kwa kuweza kufika kufanya Ibada hiyo maalum ya kuinua Biashara ya Utalii, kisha akafanya Ibada ya Kuwainua (kuwaombea) Viongozi akitangulia kumuinua Rais Dk. John Magufuli kisha wasaidizi wake wote hadi mkuu mkoa wa Arusha na Mkuu huyo wa Wilaya ya Longido.

Alisema, Kanisa Halisi wameamua kufanya Ibada hiyo kwa sababu ni wajibu wa Viongozi wa Kiroho kufanya jambo kama hilo wanapoona jambo lolote muhimu linakaribia kuathiri jamii.

"Sisi tumeamua kuifanya Ibada hii kwa kuwa tunaelekezwa na Mungu Baba kwamba ni lazima kuwa mstari wa mbele katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo kwa njia ya kufanya ibada, Linapotokea jambo lilanlotatiza watu au taifa ni lazima tuwe mstari wa mbele kutafuta kulimaliza, siyo kukaa pembeni halafu ibaki kuwalamu viongozi", alisema Baba wa Uzao.

Baba wa Uzao aliwataka Watanzania kuwa mstari wa mbele katika kutembelea vivutio vya Utalii kwenye maeneo mbalimbali badala ya kuwaachia watalii kutoka nchi za nje.


Baba wa Uzao akisindikizwa na Kaka wa Uzao kwenda meza kuu ili kuanza ibada hiyo maalum katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Meya wa zamani wa Jiji la Arusha Sheik Amri Abeid.
☝Baba wa Uzao na Mama wa Uzao pamoja na Dada wa Uzao wakiwa tayari meza kuu kuanza Ibada hiyo. Kulia ni Kaka wa Uzao.👇

MKUU WA WILAYA AKIWASILI👇
Mkuu wa wilaya ya Longido akilakiwa na Kuhani pamoja na Polisi
Kuhani na polisi wakimsindikiza Mkuu huyo wa Wilaya ya Longido kwenda Jukwaani.
Baba wa Uzao akimlaki kwa salam na bashasha Mkuu huyo wa Wilaya ya Longido.
"Karibu sana, Tumefurahi sana kuja... asante", akasema Baba wa Uzao akiendelea kumlaki Mkuu huyo wa Wilaya.

Mkuu huyo wa Wilaya akimsalimia Mama wa Uzao. 
Baada ya kulakiwa Mkuu huyo wa Wilaya akikabidhiwa Ratiba na Mlinzi wake (Polisi).
Baba wa Uzao akizungumza maneno ya utangulizi kumkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya ya Longido (kulia).
Baba wa Uzao akifanya shukrani (Maombi) kwa ajili ya Mungu Baba kuwezesha Ibada hiyo kufanyika.

Kisha Baba wa Uzao akafanya shukrani (maombi) kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli na Wasaidizi wake wote akiwemo mkuu wa mkoa wa Arusha na Mkuu huyo wa wilaya ya Longido na baadaye akamkaribisha mgeni rasmi kuzungumza.

Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha Frank Mwaisumbe akizungumza kabla ya kuanza Ibada maalum ya kufungua Biashara ya Utalii Ukanda wa Kaskazini, iliyofanywa na Kanisa Halisi la Mungu Baba la Tegeta jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha jana. Mkuu huyo wa Wilaya alimwakilisha Mkuu wa mkoa huo Iddi Kimanta kuwa mgeni rasmi. Kulia ni Mkuu wa Kanisa hilo Mama wa Uzao akiwa na Mama wa Uzao.
Baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kumaliza hotuba yake akapokewa na Baba wa Uzao wakati akirejea kuketi meza kuu.

Baba wa Uzao akasoma shukrani tena, kisha akaanza kutoa somo kueleza kwa nini Kanisa Halisi linafanya Ibada Maalum ya Kuinua Biashara ya Utalii Ukanda wa Kaskazini - Arusha.
Baba wa Uzao akiendelea kufanya shukrani kabla ya kuanza rasmi somo hilo.
☝Baada ya mgeni rasmi kuketi Baba wa Uzao akaendelea na somo.👇

Vijana wa kitengo cha Mawasiliano cha Kanisa Halisi wakiwajibika kufanikisha Ibada hiyo.
Makuhani wa Kanisa Haliai la Mungu Baba wakijadilia mambo fulani muhimu wakati wa Ibada hiyo.

Kikundi cha Burudani ya muziki wa Kumtukuza Mungu Baba cha Kanisa Halisi wakiwajibika kunogesha Ibada hiyo👇











Kanisa halisi la Mungu Baba halibagui; Kijana akiselebuka kumtukuza Mungu Baba wakati wa nyimbo za kundi hilo👇

shangwe kwa Mungu Baba👇

Baba wa Uzao akiendelea kutoa somo👇


Uzao na Makuhani wakimsikiliza na wengine wakiandika dondoo wakati Baba wa Uzao akitoa somo👇




Mkuu wa Wilaya akiagana na Baba wa Uzao kabla ya kuondoka👇
"Tunakushukuru sana Mkuu wa Wilaya, kweli tumefarijika sana. asante", akasema Baba wa Uzao wakati anaagana na Mkuu huyo wa Wilaya.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana