Na Richard Mwaikenda, Dodoma
KAMATI ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) inaanza ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa ardhi na biashara katika Wilaya za Mufindi, Mbarali na Njombe.
Akitoa taarifa ya ziara hiyo hivi karibuni jijini Dodoma, Mratibu wa Mpango huo, CPA, Dkt. Seraphia Mgembe amesema kuwa kamati ya uongozi pia itashiriki katika tukio la utoaji hati za haki miliki za kimila katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la ofisi ya masjala ya ardhi ya Kijiji cha Kapyo, Mbarali.
Amesema ziara hiyo ya wiki moja inaanza leo Jumapili Januari 24 na kumalizika Januari 31 mwaka huu.
Post a Comment