Featured

    Featured Posts

SERIKALI YATISHIA KUWANYANG'ANYA WAKULIMA WALIOHODHI MASHAMBA YA NGANO BILA KUYALIMA



Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda akizungumza kwenye kikao cha wadau wa zao la ngano kilichofanyika jijini Dodoma leo Januari 23,2021 ambapo  Wizara imeingia makubaliano na makampuni makubwa ya ngano ikiwemo Bakhresa, Azania, Sunkist, AMSONS,Jumbo, TBL na Serengeti Breweries kuanza kununua ngano ya wakulima wa kwa bei ya shilingi 800 kwa kilo.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha wadau wa ngano wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda(hayupo pichani) wakati  akizungumza kwenye kikao cha wadau wa zao la ngano kilichofanyika jijini Dodoma  Januari 23,2021
Waziri Prof. Mkenda akijadiliana jambo na Naibu waziri, Bashe.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa inayolima zao la ngano.
Mdau wa Kilimo cha Ngano kutoka Mkoa wa Ruvuma, Msigwa akieleea kero zinazowakabili wakulima wa zao hilo pamoja na kutoa maoni yake jinsi ya kuzipatia ufumbuzi.
Katib Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya akizungumza katika mkutano huo.

 Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akizungumza kwenye  kikao cha wadau wa zao la ngano kilichofanyika leo jijini Dodoma Januari 23,2021 ambapo Wizara imeingia makubaliano na makampuni makubwa ya ngano ikiwemo Bakhresa, Azania, Sunkist, AMSONS,Jumbo, TBL na Serengeti Breweries kuanza kununua ngano ya wakulima wa kwa bei ya shilingi 800 kwa kilo.


Na Richard Mwaikenda, Dodoma


SERIKALI imetishia kuwanyang'anya  wakulima waliyoyachukua mashamba ya serikali kwa ajili ya kilimo cha ngano lakini hawalimi zao hilo.


Tishio hilo limetolewa na Waziri wa Kilimo, Prof. Adolph Mkenda wakati wa kikao cha pamoja na wadau wa zao hilo cha kujadili jinsi kuamsha tena kilimo cha ngano nchini kilichofanyika jijini Dodoma Januari 23, 2021.


 "Wakulima wa ngano waliochukua mashamba ya serikali hakikisheni mnalima mashamba hayo kabla serikali haijachukua uamuzi mwingine wa kuyachukua,"amesema Waziri Mkenda huku akiahidi kwamba serikali kwa hivi sasa iko tayari kulisimamia kikamilifu kuliamsha.


 Kikao hicho kilihudhuriwa na wadau kilimo hicho kutoka mikoa mbalimbali inayostawisha zao hilo, wakuu wa mikoa ya Manyara, Arusha, Dodoma, wenye viwanda vya kuchakata ngano, wanunuzi wa zao hilo pamoja na maofisa wa serikali na taasisi zake.


Amesema Wizara ya kilimo imejidhatiti kikamilifu kuhakikisha wanafanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kutazama zao moja baada ya jingine ili kuhakikisha kero katika mazao hayo zinaondoshwa.


Prof. Mkenda amesema serikali imeweka mikakati ya kuliamsha tena zao la ngano na shayiri ili kupunguza kuagiza mazao hayo kutoka nje ya nchi, ambapo uzalishaji wa ndani ukiwa ni tani 60,000 hadi 70,000 licha ya wataalam kusema Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuzalisha ngano katika nchi za Afrika Mashariki.


Prof. Mkenda amesema kadri muda unavyo songa mbele wakulima wamekuwa wakiacha kulima ngano kutokana na  kutumia gharama nyingi lakini bei yake bado ikiwa chini.


Amesema kama Serikali wemekuwa wakifanya kila jitihada kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kutoka kuzalisha tani 0. 7 hadi tani 1 kwa ekari moja ya ngano hadi kufikia uzalishaji wa nje ambao huzalisha hadi tani 5 kwa ekari moja.


Amesema kuwa moja ya sababu inayosababisha  zao hilo kudorora ni bei kuwa chini hali inaowafanya wakulima kutokuwa na  hamasa na lakini pia kiwango cha ubora kiko chini.


"Tusipoyamaliza haya kilimo hakitakuwa endelevu, leo tunaanza safari ya kunyanyua tena zao la ngano na shayiri, kwa ngano bei tumepandisha hadi kufikia 800” amesema.


Aidha, Prof. Mkenda amesema Katika kuhakikisha inamaliza kero za wawekezaji nchini  Wizara ya Kilimo ipo mbioni kuanzisha dawati maalumu litakalotumika na sekta binafsi katika kuwasilisha kero zinazowakabili katika shughuli zao  na kwamba katika dawati hilo wataweka watu makini watakaoweza kutatua kero za wawekezaji nchini.

  


“Tutaliimarisha dawati hilo kikamilifu na watu tutakaowaweka ni watu makini kweli kweli ambao watakuwa na uwezo wa kushughulikia kero za wakulima na wawekezaji katika sekta ya kilimo” amesema Prof. Mkenda.

Wizara imeingia makubaliano na makampuni makubwa ya ngano ikiwemo Bakhresa, Azania, Sunkist, AMSONS,Jumbo, TBL na Serengeti Breweries kuanza kununua ngano ya wakulima wa kwa bei ya shilingi 800 kwa kilo.

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,  Gerald Kusaya amesema kuwa Tanzania imekuwa ikitumia trilioni 1.03 kwa ajili ya kuagiza ngano kutoka nje ya nchi kufidia upungufu uliopo.


Amesema Tanzania ina hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo lakini ni hekta milioni 10.8 ndio zinatumika hali inayopelekea ziada kuagiza nje ya nchi jambo ambalo ni aibu na halifai kulifumbia macho.


Asilimia kubwa ya wadau walioruhusiwa kuchangia mawazo na kutoa maoni yao, waliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongwa na Rais John Magufuli kwa kuweka mfumo mzuri kwa wawekezaji kufanya shughuli zao vizuri ikiwemo kuwashirikisha kwenye vikao vya kujadili kero na kuzitafutia ufumbuzi, huku wakitolea mfano wa kikao hicho.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana