Featured

    Featured Posts

MKURABITA WATETA NA RAS WALIPOWASILI KIKAZI NJOMBE+video

KAMATI ya Uongozi ya Mpango wa Urasimishaji wa Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), wamewasili mkoani Njombe na kukaribishwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Katerina Revocati ambapo walizungumzia mambo mbalimbali ya utekelezaji wa urasimishaji wa rasilimali za wanyonge mkoani humo. Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay imetinga mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa urasimshaji pamoja na kufanya vikao vya pamoja na wadau walionufaika kupata mikopo benki kwa kutumia Hati Hakmiliki za kimila kama dhamana..

Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Katerina Revocati (kulia) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Urasimishaji wa Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) walipowasili katika Ofisi za Mkoa wa Njombe Januari 28,2021. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi mstaafu Daniel  Ole Njoolay. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mratibu wa Mkurabita ambaye ni Katibu wa Kamati hiyo, Dkt Seraphia Mgembe akielezea kwa ufupi kuhusu ziara yao mkoani humo.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi mstaafu Daniel  Ole Njoolay. akizungumza jambo wakati wa kikao na RAS Revocati.
Mjumbe wa Bodi, Haji Janabi akifafanua jambo kuhusu mambo ya uwekezaji .
Mjumbe wa Bodi, akichangia jambo wakati wa mazungumzo hayo

Kaimu Mkurugeni wa Urasimishaji Ardhi na Biashara wa Mkurabita, Jane Lyimo (kushoto) akikumbatiana kwa furaha na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Revocate baada ya kukutana katika ofisi hizo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Revokati  akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mkurabita pamoja na watendaji wa Mpango huo.

RAS Revocate akiwaaga wajumbe hao
Wajumbe wakiondoka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa tayari kwenda kwa Mkuu wa Wilaya Njombe kukutana naye.
Wajumbe wa Bodi ya Mkurabita, wakiwa katika kikao na Kaimu Tawala wa Wilaya Njombe,Nganyagwa Erneo ambapo walitoa utambulisho na kuelezea kuhusu madhumuni ya ziara yao.


Wajumbe wakiondoka katika Ofisi za Wilaya ya Njombe kuendelea na ziara yao wilyani humo.

Mdau nakuomba uendelee kusikiliza yaliyojiri kwenye kikao hicho kupitia kwenye clip hii ya video...
 


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana