Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Jioloji wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dkt. Michael Msabi akishiriki kupanda miti.
Diwani wa Kata ya Mbabana, Paskazia Mayala akipanda mti katika eneo la shule.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Mbabana, Hezron Lupondo akipanda mti. Pia ni mwalimu wa shule hiyo.
Mnec Sinene akitoa maelekezo jinsi ya kupanda miti.
Na Richard Maikenda, Dodoma
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), Ahidi Sinene hadi sasa amehamasisha wananchi kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti 700 katika Kata mbalimbali jijini Dodoma.
Kila anapokwenda kupanda miti amekuwa akihamasisha kila mwananchi kuwajibika kupanda angalau kwa uchache miti mitano katika eneo lake kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani.
Januari 16, 2021, Mnec Sinene alikwenda kushiriki kupanda miti katika Shule ya Sekondari Bihawana, Kata ya Mbabana nje kidogo ya Jiji la Dodoma ambapo walipanda miti 230 ikiwemo ya matunda.
Katika kazi hiyo ya upandaji miti, Sinene alisema anaunga mkono agizo la Makamu wa Rais Samia Suhuhu Hassan la wananchi kupanda miti kuhifadhi mazingira ambapo alishirikiana na viongozi wa chama na serikali wa kata hiyo, walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.
Aliwahimiza walimu na wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha miti iliyopandwa inahudumiwa ipasavyo, pia waweke utaratibu wa kila mgeni anayetembelea shuleni hapo awe anapanda mti utakaowekewa lebo ya jina lake kwa ajili ya kumbukumbu.
Kwa Taarifa Zaidi endelea kusikiliza Clip hii ya video…
Post a Comment