RC Mahenge akitoa shukrani kwa watu wote waliojitokeza kupanda miti katika eneo hilo Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Josephat Maganga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Chuo Kikuu cha Dodoma, Kitivo cha Elimu, Godfrey Masele akipanda mti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru akielezea historia ya eneo la wazi la Iseni Park na jinsi litakavyoboreshwa kwa kupanda miti na kuitunza ili kuifanya bustani hiyo kuwa ya kuvutia.
Mratibu wa Wakala wa Barabara Vijijini, Mhandisi Lusako Kilembe akielezea jinsi watakavyopanda miti kwenye barabara wanazozijenga jijini Dodoma. Katikati ni Mjume wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Ahidi Sinene.
Dkt Mahenge amesema ni wajibu kwa kila mtanzania kuona umuhimu wa kupanda miti katika maeneo yao kwani ndio ulithi pekee tulioachiwa katika sayari hii.
“Tangu sayari hii iumbwe haiongezeki wala kupungua ndio tunayoishi na rasilimali tulizo achiwa na zinazidi kupungua, mito mingi inakauka ni wajibu wetu kuendelea kulinda” amesisitiza Dkt. Mahenge.
Amesema katika kuendelea kwa Teknolojia hapa Duniani zimeathiri uoto wa asili, ili kurudisha uasilia wa uoto wa asili ni lazima kutunza mazingira na kuendelea kupanda miti katika maeneo yaliyo wazi.
Amewataka watanzania kuendelea kuhamasika katika kulinda mazingira na kujenga utamaduni wa kupanda miti katika maeneo yote hasa katika maeneo ya Mkoa wa Dodoma.
Wakati huo huo, Meneja wa TFS, Kanda ya Kati, Mathew Kiondo amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Mahenge aje azindue kampeni ya umwagiliaji wa miti iliyopandwa hasa wakati wakiangazi ili istawi vizuri.
Kiondo ameomba ushirikiano na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), kuweka matanki ya maji eneo hilo kwa ajili ya umwagiliaji kwenye miti hiyo.
Post a Comment