RAIS DK. HUSSEIN MWINYI NA MAALIM SEIF WASHIRIKI TAMASHA LA MAZOEZI YA VIUNGO ZANZIBAR, LA KILA JANUARI MOSI.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na wakishiriki katika mazoezi ya pamoja ya viungo yakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Omar Hassan King, baada ya kumaliza matembezi ya mazoezi hayo katika viwanja vya Amaan Jijini Zanzibar, wakati wa Tamasha la Kitaifa la Mazoezi ya Viungo Zanzibar lililofanyika leo 1-1-2021. (Pichani na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhi Cheti cha Heshima kwa Mshiriki namba moja wa Mazoezi Zanzibar, Mwenyekiti wa Chama Cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) Said Suleiman, wakati wa hafla ya mazoezi ya viungo ya pamoja yaliofanyika katikia Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar leo 1-1-2021. Zifuatazo ni pichani mbalimbali za mazoezi hayo👇
Post a Comment