Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI David Silinde amemvua madaraka Mkuu wa Shule ya Lulumba Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na kuagiza Afisa Elimu Sekondari kuandika maelezo ya kwanini jengo la bweni halijakamilika kwa wakati huku fedha zikiwa zimepelekwa toka mwezi wa sita mwaka 2020 na ikitakiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu.
Pia Silinde amevunja Kamati ya Ujenzi ya Shule hiyo kwakushindwa kusimamia, hatua hiyo ameichukua baada ya kufanya ukaguzi wa fedha za mradi wa lipa kulingana na matokeo (EP4R) kwa kuboresha utoaji wa elimu nchini.
Post a Comment