Featured

    Featured Posts

UN YAKARIBISHA KUANZA KUKELEZWA MKATABA UNOPIGA MRUFUKU SILAHA ZA NYUKLIA

UN yakaribisha kuanza kutekelezwa mkataba unaopiga marufuku silaha za nyuklia

Kuwepo maghala ya silaha za nyuklia duniani na kuongeza na kustawisha pakubwa silaha hizo na pia kujiunga serikali mpya na klabu ya nyuklia kumeibua matarajio yasiyofaa kwa amani na usalama wa kimataifa. Jambo hili limepelekea kutoepukika udharura wa kufikiwa mkataba mpya kwa jina la Mkataba wa Kupiga Marufuku Silaha za Nyuklia yaani The Treaty on the Prohibition of Nuclear Weapons (TPNW) ambao ulipasishwa mwezi Julai mwaka 2017.

Mkataba huo wa Kupiga Marufuku Silaha za Nyuklia umeanza kutekelezwa tangu jana Ijumaa tarehe 22 Januari 2021 bila ya kusainiwa na nchi kubwa zinazomiliki silaha za nyuklia duniani, lakini umeungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa taarifa na na kulitaja suala hilo kuwa ni hatua muhimu kuelekea kwenye ulimwengu usio na silaha za nyuklia. Ameongeza kuwa: huu ni mkataba wa kwanza wa pande kadhaa unaopiga marufuku silaha za nyuklia ambao ulifikiwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita. 

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa UN  

Mkataba wa Kupiga Marufuku Silaha za Nyuklia unazuia matumizi, uenezaji, uundaji, kuzifanyia majaribio, kulimbikiza na kutishia kutumia silaha za aina hiyo. Mkataba huo umetekelezwa siku 90 baada ya kupasishwa na nchi ya 50 iliousaini yaani tarehe 22 mwezi huu wa Januari. Hadi sasa nchi 80 ndizo zilizosaini mkataba huo; na nchi 51 pia duniani zimeupasisha katika mabunge yao. Wanaharakati wanaopinga matumizi ya silaha za nyuklia duniani na nchi zilizosaini mkataba wa TPNW zinataraji kuwa mkataba huo utakuwa na taathira bila hata ya kuungwa mkono na madola yanayomiliki silaha za nyuklia na utakuwa kigezo cha kufuata ili uweze kubadili kabisa mitazamo ya madola yanayomiliki silaha za nyuklia duniani.  

Lengo kuu la mkataba huo ni kuanzisha kanuni ya kisheria ya kuwalaumu na kuwakosoa wamiliki wa silaha za nyuklia, pamoja na kuzidisha mashinikizo ili nchi zinazomiliki silaha za atomiki duniani zitekeleze majukumu yao ya kuangamiza silaha hizo. Pamoja na kuwepo Mkataba wa Kuzuia Unezaji wa  Silaha za Nyuklia yaani Non-Proliferation Treaty (NPT) ambao ulipasishwa mwaka 1968; na kuanza kutekelezwa mwaka 1970 lakini si tu hakuna hatua yoyote ya maana iliyochukuliwa hadi sasa kwa ajili ya kupunguza maghala ya silaha za nyuklia bali ni wazi kuwa nchi zilizojilimbikizia silaha hizo zimeongezeka huku ukiongezeka pia ushindani wa kuwa na silaha hatari na angamizi zaidi na za kisasa zaidi za atomiki duniani. 

Mkataba wa NPT unaozuia uenezaji wa silaha za nyuklia 

Madola makuu ya nyuklia duniani yanapinga vikali Mkataba wa Kupiga Marufuku Silaha za Nyuklia. Hakuna hata nchi moja kati ya zinazomiliki silaha za atomiki iliyosaini mkataba huo na hata zimesusia mazungumzo ya kupasisha mkataba huo. Mbali na Marekani na Russia ambazo zinamiliki asilimia 90 ya silaha za nyuklia duniani; Ufaransa, China, Uingereza, India, Pakistan, Utawala wa Kizayuni wa Israel na Korea ya Kaskazini pia ni nchi nyingine zinazomiliki silaha za nyuklia duniani. Marekani, Ufaransa, Uingereza, China na Russia mwezi Oktoba mwaka 2018 ziliatoa taarifa ya pamoja na kueleza kuwa zinapinga Mkataba wa Kupiga Marufuku Silaha za Nyuklia na kwamba hazitautia saini mkataba huo. Nchi hizo zinadai kuwa mbinu mkataba wa hivi sasa wa NPT unatokasha kwani zinadai umefanikiwa kikamilifu kupunguza maghala ya silaha za nyuklia duniani. Nchi hizo zinaamini kuwa, Mkataba huu mpya utakinzana na ule wa NPT na unaweza pia kuathiri mkataba huo.   

Hata hivyo, Beatrice Fihn, Mkurugenzi wa Harakati ya International Campaign to Abolish Nuclear Weapons amepinga madai ya nchi hiyo kwamba Mkataba wa Kupiga Marufuku Silaha za Nyuklia (TPNW) utapelekea kudhoofika mkataba wa NPT na kusisitiza kuwa: mkataba huo unakwenda sambamba na lengo la kuu la NPT.  

Kwa miongo kadhaa sasa ulimwengu unakabiliwa na jinamizi la vita vya nyuklia; na silaha hizo ni tishio kuu kwa amani na usalama wa kimataifa hasa kwa vile kuna maelfu ya silaha za nyuklia katika maghala ya madola makubwa yanayomiliki silaha hizo hatari duniani huku baadhi ya nchi zikifanikiwa kumiliki silaha hizo angamizi katika miongo kadhaa ya karibuni. 

Maafa angamizi ya silaha za nyuklia duniani 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana