Featured

    Featured Posts

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZISHI YA ROSEMARY NYERERE


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiweka shada la maua katika kaburi la Rosemary Nyerere ambaye ni Mtoto wa Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambara Nyerere katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo katika Kituo cha Hija Pugu Jijini Dar es Salaam, leo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameshiriki mazishi ya mtoto wa Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rosemary Nyerere aliyefariki dunia Januari Mosi, 2021.

Mazishi hayo ya Rosemary Nyerere yamefanyika leo  katika makaburi ya Kanisa Katoliki yaliyopo kwenye Kituo cha Hija kilichoko Pugu jijini Dar es Salaam.

Ibada ya mazishi imeongozwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki Upanga jijini Dar es Salaam, Dias Mario.

Viongozi wengine walioshiriki katika mazishi hayo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Mama Sitti, Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba.

Wengine ni mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula.

Viongozi wengine ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi, Spika Mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakary Kunenge na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana