Featured

    Featured Posts

BILLIONEA WA MADINI YA RUBY AISHUKURU SERIKALI

 

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Billionea wa madini ya Ruby,Gabriel Sendeu Laizer anayefanya shughuli zake za uchimbaji kata ya Mundarara Wilayani Longido ameishukuru ameishukuru   serikali kupitia wizara ya madini pamoja na tume ya madini kwa kutambua mchango wake  katika sekta ya madini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Arusha Sendeu ambaye alibuka kuwa billionea katika sekta hiyo baada kupata tani tano za madini ya ruby yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.7 alisema kuwa anaishukuru serikali kutambua kazi anayoifanya kwa kumpa cheti cha kutambua mchango wake pamoja na zawadi  alizopewa katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini 2021 ambao uliofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere.
Sendeu alisema  kuwa mafanikio  aliyoyapata ni matokeo ya hatua zinazochukuliwa na serikali  ya kuwajengea wachimbaji wadogo mazingira mazuri ya kufanya shughuli za uchimbaji hivyo pamoja na kutambua mchango wake pia anaishukuru kwa hilo.
“Naishukuru sekta ya madini na serikali hususani Rais John Magufuli kwa kututhamini wachimbaji wadogo na kututetea hatua ambayo ndio inayochangia mafanikio yangu kwa sasa na sio vinginevyo,”Alisema Sendeu.
Pamoja na hayo pia aliwashauri wachimbaji wenzake wadogo wa madini kuendelea kuchimba bila kukata tamaa kwani kazi hiyo inahitaji uvumilivu na kujitoa pamoja na  kutoa ushirikiano kwa serikali ikiwemo kudhibiti utoroshaji wa madini ili yaendeleee kuwanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana