Featured

    Featured Posts

WAZIRI MKUU AZINDUA MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI SINGIDA

 


WAZIRI
anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Singida kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Angelina Lutambi

 


Kikundi cha Ngoma Asili cha Sarakasi wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo huo




WAZIRI wa Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikagua baadhi bidhaa zilizoletwa na wadau mbalimbali

Kwaya ya Chuo cha Utumishi Singida wakitumbuiza wakati wa tukio hilo


Na John Mapepele, Singida

Waziri
kuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassimu Majaliwa amezitaka  Mamlaka zote za Mikoa  kujipanga kikamilifu kutangaza fursa za uwekezaji zinapatikana kwenye  mikoa yao kwa kushirikiana Kituo cha 
Taifa  cha Uwezekezaji  ili kuhakikisha kuwa fursa zote zilizoainishwa kwenye  miongozo ya  uwekezaji  zinapata wawekezaji makini ili kuongeza mapato na ajira kwa wananchi

 Akisoma  hotuba  ya Mheshimiwa
Waziri Mkuu kwenye  tukio la uzinduzi wa Mwongozo wa Fursa za Uwekezaji Mkoa wa Singida,   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo  wa miaka  mitano(5) Serikali imedhamilia  kuimarisha  ustawi wa wananchi wake  kwa kuzalisha ajira  milioni nane na kukuza uchumi wake kwa asilimia nane  hivyo uwekezaji  makini unatakiwa ili kufanikisha azma hiyo.

Amesema  ili kuwapata wawekezaji makaini watendaji wote wa Serikali hawana budi kutoa taarifa sahihi za fursa zinazopatikana  katika maeneo yao na utaratibu wote wa  namna ya  kuufuata ili kuweza kuwekeza.

“Ndugu zangu ni muhimu sana tubadilike  taarifa za  uwekekezaji tunazozitoa ziwe  sahihi na ziwe zinafanana, ukienda kwa Mkuu wa  Mkoa upate taarifa sawa na ukichukua taarifa hiyo kwa  Katibu Tawala wa Mkoa na Mkurugenzi
Mtendaji wa  Halmashauri hapo tutakuwa tumefanikiwa” amesisitiza Profesa Mkumbo.

Amezitaka  mamlaka hizo kutowakwamisha 
wawekezaji kwa  kuhakikisha  maeneo ya uwekezaji  yanapatikana mara moja ili pindi Wawekezaji wanapofika wanapatiwa   maeneo hayo na wanahudumiwa  kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto zozote
zinazojitokeza.

Amesema  balozi  namba moja  anayeweza kuleta au
kutoleta wawekezazi katika nchi yoyote  duniani ni Muwekezaji aliye ndani ya nchi husika  hivyo  ni muhimu  kuwapa huduma  bora  ili waweze kutuletea wawekezaji wengi zaidi ambapo amesisitiza  uwekezaji ufanywe kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya  Serikali ili nchi yetu iweze kunufaika.

Amekemea tabia  ya kupenda kutoa lawama  baada
ya  kuingia mikataba  mibovu na wawekezaji na badala yake amewataka 
watendaji kuwa makini katika  mchakato mzima wa majadiliano na kufunga
mikataba hiyo na wawekezaji.

Aidha, ameitaka  kila Mkoa kuangalia
kuangalia maeneo  machache ya kipekee ili kufanya uwekezaji  wenye tija
badala ya kwenda na maeneo mengi ambayo  hayana  tija.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais John Pombe
Magufuli kwa kubuni mikkakati  kabambe ya uwekezaji ambayotayari katika kipindi kifupi imeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii kwenye nchi yetu.

Amesema Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa ambayo
ilikuwa ikionekana kama  mikoa masikini lakini sasa  umekuwa  ni miongoni mwa mikoa ambayo inaweza kuongoza  kuleta  mapato makubwa kwa nchi  kutokana na  kuboreshwa kwa  mazingira na fursa nyingi zilizopo.

Ametaja baadhi ya fursa za uwekezaji  zinazopatikana kuwa ni pamoja na madini,kilimo  cha Alizeti na Korosho, mafuta asilina na gesi pia elimu.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana