Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anna Abdallah na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa uongozi wa Chuo Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School), yeye na ujumbe wake walipotembelea chuo hicho, Kibaha mkoa wa Pwani, jana.
Kibaha, Pwani
Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anna Abdallah amesema katika Chuo Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School) ndipo mahala rasmi ambapo sasa zile fikra zake za kulikomboa Bara la Afrika zitatekelezwa kwa vitendo kwa sababu watapatikana viongozi ambao watakuwa na uzalendo wa hali ya juu kwa kuwa mafunzo watakayopata hapo yataakisi na yataelekeza Itikadi na falsafa za Mwalimu Nyerere.
Mama Anna Abdallah alisema hayo, jana wakati yeye na Wajumbe wa Baraza hilo walipo walitembelea Chuo hicho kilichopo eneo la Kibaha katika mkoa wa Pwani kwa ajili ya kujionea ujenzi wa kisasa uliofanyika na kushuhudia mambo mbalimbali kabla ya kuanza kwa masomo ya Uongozi katika chuo hicho..
"Sote tumeshuhudia hata baadhi ya watoto wa Viongozi ambao wamelelewana kuishi maisha yao yote ndani ya CCM, kuwa ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kusema mabaya kuhusu nchi ya Tanzania na kuharibu taswira ya nchi hii, hayo yataondoka kwa watu kuja kujifunza uzalendo katika chuo hiki , kwa sababu kiongozi mzuri anajengwa na kufundishwa Uzalendo wa Taifa lake.
Jina la Mwalimu Julius Nyerere limetumika katika maeneo mengi, lakini katika Chuo hicho ndipo mahala rasmi ambapo sasa zile fikra zake za kulikomboa Bara la Afrika zitatekelezwa kwa vitendo kwa sababu watapatikana viongozi ambao watakuwa na uzalendo wa hali ya juu kwa kuwa mafunzo watakayopata hapo yataakisi na yataelekeza Itikadi na falsafa za Mwalimu Nyerere", alisema Mama Anna.
Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Baraza hilo Mama Anna Abdallah aliongozana na Wajumbe wa Baraza ambao ni Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Pandu Omer Kificho, Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Kepteni Mstaafu John Chiligati, Charles Singili na Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay.
Wengine kwenye Msafara huo walikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Bara Rodrick Mpogolo ambaye ndiye Katibu wa Sekretalieti ya Baraza hilo la Wadhamini wa CCM, Katibu wa NEC - Uchumi na Fedha Zanzibar Afadhali Afadhali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mwalimu Raymond Mwangwala ambaye pia ni Mjumbe wa NEC.
Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anna Abdallah na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chuo Uongozi cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Julius Nyerere Leadership School), baada ya kutembelea chuo hicho, jana, Kibaha mkoa wa Pwani, jana.
Post a Comment