Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akionesha tuzo aliyokabidhiwa na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kinondoni kwa kutambua mchango mkubwa alioutoa kwa Chama katika mkoa huo, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 44 ya CCM yaliyofanyika leo Febuari 06, 2021 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabwepande Wilayani humo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akipokea tuzo aliyokabidhiwa na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kinondoni kwa kutambua mchango mkubwa alioutoa kwa Chama katika mkoa huo, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 44 ya CCM yaliyofanyika leo Febuari 06, 2021 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabwepande Wilayani humo. Anayemkabidhi ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Harold Maruma.
Baadhi ya Viongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wana CCM na wananchi kwa jumla wakiwa kwenye hafla hiyo
Mmoja wa Makada wa siku nyingi wa CCM, akifuatilia hali ya mambo wakati wa hafla hiyo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisalimia wananchi alipowasili kuongoza Maadhimisho ya Miaka 44 ya CCM yaliyofanyika leo Febuari 06, 2021 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabwepande Wilayani humo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Harold Maruma.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akipanda mti wakati wa Maadhimisho ya Miaka 44 ya CCM yaliyofanyika leo Febuari 06, 2021 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabwepande Wilayani humo.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Jengo la Hospitali ya Kisasa ya Wilaya ya Kinondoni katika eneo la Mabwepande Jijini Dar es Salaam, leo Febuari 06, 2021. kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba.
Jengo la Hospitali ya Kisasa ya Wilaya ya Kinondoni katika eneo la Mabwepande Jijini Dar es Salaam, ambalo ujenzi wake unaendelea. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Post a Comment