Sabuni iliyotengenezwa kwa mchele
Mkurugenzi wa Zaidat inayoundwa na wajasiriamali 6, Tatu Seleman akizungumza na vyombo vya habari kuhusu bidhaa malimali wanazotengeneza.
Wajumbe wa Bodi na watendaji wa Mkurabita wakipata maelezo kuhusu uora wa sabuni na vipodozi vyao.
Na Richard Mwaikenda, Zanzibar
WAJUMBE wa Kamati ya Uongozi na watendaji wa Mpango wa Kurasimisha Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), wametembelea kikundi cha Zaidat Products Zanzibar wanufaika wa mpango huo wanaotengeneza aina mbalimbali za sabuni na vipodozi vya asili.
Baadhi ya sabuni wanazotengeneza katika kiwanda chao kilichopo Chukwaani, Unguja Zanzibar ni; ya mchele, kahawa, mkaratusi, mwani, tangawizi pamoja na vipodozi vyake.Wajume wa Mkurabita walifurahishwa uzalishaji wa bidhaa hizo za asili hku wengine wakinunua kwa matumizi yao binafsi.
Imeandaliwa na; Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
Post a Comment