Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali, Wafanyakazi wa Mahakama, Majaji pamoja na wananchi wa mkoa wa Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini na miaka 100 ya Mahakama Kuu yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma leo Februari 1,2021.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma akizungumza cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini na miaka 100 ya Mahakama Kuu yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma leo tarehe 1 Februari 2021.
Baadhi ya Majaji wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akisoma hotuba yake katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini na miaka 100 ya Mahakama Kuu yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali mkoani Dodoma leo tarehe 1 Februari 2021.
…………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
RAIS John Magufuli ametaka lugha ya Kiswahili kuanza kutumika katika masuala ya kimahakama na kisheria katika ngazi zote.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Februari 1,2021 jijini Dodoma wakati akifunga kilele Cha siku ya Sheria nchini iliyoambatana na maadhimisho ya Miaka 100 ya Mahakama huku akieleza kuendelea kwa vitendo vya rushwa kwa baadhi ya watumishi,hivyo ni vyema wale wachache wanaoichafua Mahakama wakaanza kuchukuliwa hatua.
Rais Magufuli amesema kuwa Kiswahili kinatumika AU,SADC na EAC sioni sababu ya kwanini Mahakama hamataki kutumia Kiswahili.
“Jaji mkuu hapa amezungumza Kiswahili kizuri kuliko changu cha Kisukuma lakini ukienda kuhukumu unaandika kingereza,hicho Kiswahili kimepotelea wapi,hii ni changamoto kubwa lazima tubadilike na tukipende kilicho chetu”amesema.
Wakati huo huo Rais amewaagiza wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya wote kuhakikisha kamati za maadili zinakutana mwezi huu wa pili nakupatiwa ripoti wamekutana mara ngapi.
“Nimesikia kuwa kamati za maadili za maofisa wa Mahakama wa Mikoa na Wilaya ambazo kisheria zinaongozwa na ma RC na DC hazikutani,wamepewa madaraka ili kushughulikia masuala ya maadili lakini hawakutani na kupelekea kushindwa kuchukua hatua kwa watumishi wenye mkosa.
Wakati mwingine unaweza kulaumu huku kumbe waliopewa madaraka ya kusimamia wamekaa kimya”amesisitiza Rais Magufuli
Aidha amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni kasi ya usikilizaji kesi imeongezeka sana na tatizo la mlundikano wa kesi au mashauri limepungua kwa kiasi kikubwa,
“Mwaka 2020 Mahakama za Mwazo ilisikiliza mashauri lak 1,064,758 na mlundikano yani kazi zilizokaa zaidi ya miezi 6 zilikuwa 29 , Mahakama zawilaya zilisikiliza mashauri 43,149 wakati mashauri yenyezaidi ya miezi ya 12 ulikuwa asilimia 18”alisema.
Kwa upande mwingine Rais Magufuli amempandisha cheo Jaji wa Mahakama kuu Kanda ya Musoma Zefrine Galeba na kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa baada ya kuonyesha uzalendo wa kutumia lugha ya Kiswahili katika kutoa hukumu kwenye kesi ya North Mara Gold Mine dhidi ya Gerald Nzumbi.
Kwa upande wake JajI Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Hamisi Juma amesema kuwa mahakama ya Tanzania katika karne ya 21 ilirithi changamoto ya uhaba mkubwa na uchakavu wa majengo Katika ngazi zote za mahakama
Naye Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kuwa wao kama bunge wanaahidi kutoa ushirikiano wa kila aina pale watakapo hitajika na wanajitahidi sana ndani ya Bunge na nje ya Bunge kuhakikisha kuwa muhimili wa Mahakama unaheshimiwa na watahakikisha wanapokuwa wanafanya kazi zao hawavuki mstari na wanajitahidi kuwa ndani ya wajibu ule ambao wamepewa na bunge kwenye katiba.
“Jukumu mlilonalo mahakama pamoja na mambo mengine kutoa haki ni jukumu zito sana,ukipewa kazi ya kutoa haki lazima uwe na hofu ya Mungu na usipokuwa nayo basi utapata tabu kama siyo duniani basi mbele ya safari”amesema Ndugai.
Wakati mwinginje Mahakama inataka kufanya kazi yake lakini kesi zinaahirishwa kwa sababu tu upelelezi unaendelea,haki inayocheleweshwa nikama haki inayokosekana.kundi hili likifanya kazi yeke vizuri basi mashauri mengi yataisha kwa wakati.
Post a Comment