Featured

    Featured Posts

video: MNAOMDODOSA RAIS ASEME KUHUSU CORONA NYAMAZENI-ASKOFU DKT CHANDE

 Na Richard Mwaikenda, Dodoma

ASKOFU Dkt. Evance Chande wa Kanisa la EAGT Nazareth la Ipagala, jijini Dodoma, amekemea na kuwataka wanyamaze wale wote wanaosemasema kwamba Rais John Magufuli haongei kuhusu hali ya Corona nchini. Askofu Dkt.Chande alitoa karipio hilo wakati wa ibada maalumu ya kuitikia wito wa maombi dhidi ya janga la corona uliotolewa na Rais Magufuli kwa kuwataka viongozi wa dini zote na wananchi kwa ujumla kufanya maombi kwa Mungu autokomeze ugonjwa huo nchini. "Wapo wengine wameanza kusemasema maneno kwamba mbona rais haongei, wanataka aongee nini? wakati tangu mwanzo alishasema tuchukue tahadhari, hajawahi kutengua hiyo kauli, sasa wewe unataka tangazo la pili la nini? Biblia inasema kuna wakati wa kusema na wakati wa kunyamaza... Na nyinyi mnaosemasema kwamba Rais haongei mnyamaze, mnaongea nini kwani yeye haoni? kwani hajui? yeye ndiyo ana taratibu zote za nchi hii anajua,iwe Dodoma, Korogwe, hata Mwanza anajua, sasa kwanini mnasemasema? Na Rais akisema sema mtazoea maneno yake, ni bora alivyosema kidogo tu inatosha," alihoji Askofu Dkt. Chande. Pia, Askofu Dkt. Chande amekemea kitendo cha baadhi ya mataifa ya nje kueneza kwenye mitandao mambo ya uongo kuhusu hali ya Corona nchini na kuhoji kuwa hivi anayeijua vizuri hali ilivyo ni mtu wa hapa nchini au kutoka nje? Amesema lengo lao kuu la mataifa hayo ni kuwajaza hofu wananchi ili washindwe hata kwenda kazini uchumi wa nchi udidimie, hivyo amewaasa wananchi kuachana kabisa na habari hizo za uongo na kuwataka wachape kazi pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na janga hilo la corona bila kusahau kumuomba Mungu. "Nampongeza sana Rais Magufuli kwa ujasiri wake na kumtegemea Mungu wakati wote linapotokea tatizo la kitaifa, hivyo mimi kama kiongozi wa dini, naunga mkono wito wake wa kututaka kama taifa kumuomba Mungu kwa siku tatu," amesema Askofu Dkt. Chande. Mdau ili nisimalize yote aliyoyazungumza kwenye ibada hiyo maalumu ya maombi kwa Mungu dhidi ya janga hilo, nakuomba uendelee kumsikiliza Askofu Dkt. Chande na waumini wake kupitia kwenye clip hii ya video...
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana