Featured

    Featured Posts

DKT. KABATI ATOA MSAADA WA MIGUU BANDIA KWA WATU 51 WENYE ULEMAVU MKOA WA IRINGA

NAIBU waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akikabidhi  miguu bandia kwa watu wenye ulemavu katika hafla iliyoandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Dk. Ritha Kabati (wa pili kulia), ambaye pia amewezesha kupatikana kwa miguu hiyo.





NAIBU waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akihutubia baada ya kukabidhi msaada huo.

Dkt. Kabati akizungumza wakati wa hafla hiyo.


Na Mwandishi Wetu, Iringa

NAIBU waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga ametoa wito kwa makampuni na Taasisi kuweka utaratibu wa kuweka gawio la faida yao ya mwaka kwa kutenga kiasi kidogo kwaajili ya watu wenye ulemavu .


Wito huo ameutoa lea februari 19, 2021 Mjini Iringa katika hafra ya kukabidhi miguu bandia kwa walemavu zaidi ya 50 kutoka katika kampuni ya Camal group kwa kushirikiana na Mbunge wa Viti maalum (CCM) Rita Kabati ambapo amesema licha ya jitihada kubwa inayofanywa na Serikali katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanaangaliwa kwa karibu na kupatiwa huduma stahiki pia wadau wana mchango mkubwa katika kuisaidia Serikali kufikia malengo yake.


Aidha Mhe. Nderiananga ameongeza kuwa watu wenye ulemavu wakipatiwa vitendea kazi hasa viungo bandia wanaweza kujisimamia wenyewe kwenye shughuli za uzalishashi mali na kujiongezea kipato kitakachowawezesha kukidhi gharama za maisha na hivyo kuwafanya kuweza kujitegemea.


“watu wenye ulemavu wana mahitaji mengi hasa viungo bandia kama miguu hivyo pamoja na jitihada kubwa ya Serikali yetu ya awamu ya tano ya kuwasaidia ndugu zetu wenye ulemavu pia ipo nafasi kwa makampuni kuweka utaratibu wa kuweka gawio la faida yao yam waka kwa kutenga kiasi kidogo kwaajili ya watu wenye ulemavu” Amesema Mhe. Ummy Nderiananga.


Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Rita Kabati amewataka watu wenye ulemavu Mkoani humo kutokuwa wanyonge kutokana na  hali waliyokuwa nayo kwani ulemavu sio mwisho wa maisha nakwamba ataendelea kuweka juhudi zote kuhakikisha watu wote wenye ulemavu Mkoani humo wanafikiwa na kupatiwa msaada ili waweze kujitegemea na kuendesha Maisha yao.


Ameongeza kuwa kwa kuliona hilo amefungua NGO itayofanyakazi kwenye maeneo ya Mikoa ya Nyanda za juu Kusini kushughulikia masuala yote ya watu wenye ulemavu hivyo ataweza kuwa na wigo mpana wa kuwafikia watu wengi zaidi na kuwasaidia.


“Mheshimiwa Naibu Waziri katika kuhakikisha nawafikia watu wengi wenye ulemavu na kuwasaidia nimefungua NGO itakayofanya kazi kwenye Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ili kushughulikia kwa ukaribu matatizo ya watu wenye ulemavu sambamba na kuwawezesha kwenye mahitaji yao ya kijamii” amesema Rita Kabati.


Awali akizungumza kwenye hafla hiyo mratibu wa zoezi hilo kutoka Kampuni ya Kamal Group Stella amesema kuwa Kampuni yao imekuwa ikifanya zoezi hilo mara kwa mara nakwamba katika Mkoa wa Iringa walipanga kuwafikia walengwa 51 licha ya kuandikisha wahitaji wengie zaidi ya 30 wakati wa kutekeleza zoezi hilo lakini mpango wa kampuni hiyo ni kugawa miguu Bandia 200 kwenye Baadhi ya Mikoa na Wilaya za Tanzania Bara.


“Sisi kama Kamal Group tunatekeleza zoezi hili kwenye Mikoa na wilaya Kadhaa za hapa Nchini na hapa Iringa tunamshukuru Mungu zoezi limeenda vizuri, tuna mshukuru Mbunge Rita Kabati kwanamna alivyoweza kufanyakazi ya kuwapata hawa ndugu zetu wenye ulemavu na leo tumeweza kuwa nao na kuwapa msaada wa miguu hii Bandia” amesema Stella.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana