Baadhi ya wanufaika wa Mkurabita wakionesha hatimiliki zao
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita, Immaculata Senje akiwaasa wanufaika hao kuzitumia hatimiliki zao kukopea fedha benki kuanzisha miradi ili kujikwamua kiuchumi badala ya kuzifungia kabatini.
Mratibu wa Mkurabita, Dk. Seraphia Mgembe akiwahamasisha wanufaika hao kuchangamkia fursa hiyo kama Tanzania Bara wanavyonufaika na hatimiliki hizo kwa kukopa fedha benki kuanzishia miradi.
Na Richard Mwaikenda, Zanzibar
VIONGOZI wa Mpango wa Kurasimisha Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), hivi karibuni wamewapiga msasa wananchi wa Shehia ya Welezo Zanzibar jinsi ya kutumia hati za Hakimiliki walizokabidhiwa kukopea fedha benki za kuanzishia miradi ili kujikomboa dhidi ya umasikini. Walioendesha mafunzo hayo ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya Uongozi wa Mkurabita, Immaculata Senje na Mratibu wa Mkurabita ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo, Dk. Seraphia Mgembe ambapo pamoja na mambo mengine waliwataka wanufaika hao wa Mkurabita kutozifungia kabatini hati hizo bali wazitumie ili kumsaidia Rais wa Zanzibar, Dk. Husseini Ali Mwinyi katika harakati zake za kuwakwamua kiuchumi kupitia uchumi wa bluu. Mdau ili nisimalize yote waliyoyazungumza, nakuomba uendelee kusikiliza yaliyojiri kwenye mafunzo hayo kupitia kwenye clip hii ya video...
Post a Comment