MABINGWA watetezi, Simba SC wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Februari 7 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kiungo Clatous Chama aliikosesha timu yake bao dakika ya 37 baada ya mkwaju wake wa penalti kuokolewa na kipa Mganda kufuatia Miquissone kuchezewa rafu Mnyarwanda, Ally Niyonzima kwenye boksi.
Kwa Matokeo hayo Simba ifikishe pointi 39 baada ya kucheza mechi 17 na kuendelea kukamata nafasi ya pili, nyuma ya watani wao wa jadi, Yanga SC wenye pointi 44 za mechi 18 huku Azam FC inafikisha pointi 33 na inabaki nafasi ya tatu, ikiwazidi pointi nne Biashara United ya Mara baada ya timu zote kucheza mechi 18.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’’, Ibrahim Ame, Pascal Wawa, Thadeo Lwanga, Percet Chikwende/Bernard Morrison dk70, Rally Bwalya/Chriss Mugalu dk77, Meddie Kagere, Clatous Chama na Luis Miquissone/Muzamil Yassin dk86.
Azam FC; Mathias Kigonya, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Daniel Amoah, Aggrey Morris, Ally Niyonzima/Yahya Zayd dk62, Ayoub Lyanga, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Mudathir Yahya dk62, Prince Dube/Never Tigere dk90, Obrey Chirwa na Iddi Suleiman ‘Nado’.
Post a Comment