Featured

    Featured Posts

VIONGOZI WA AFRIKA LEO WANAKUTANA KUJADILI CORONA

 

  • Viongozi wa Afrika leo wanakutana kujadili corona, usalamaViongozi wa bara la Afrika leo wanashiriki katika Mkutano wa 34 wa Kilele wa Umoja wa Afrika kujadili masuala ya usalama na janga la corona au COVID-19.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kabisa katika historia kwa mkutano wa kilele wa viongozi wa Afrika kufanyika kwa njia ya intaneti kutokana na hofu ya kuenea ugongjwa wa corona.

Katika mkutano huo wa siku mbili, viongozi wa Afrika pia wanatazamiwa kumchagua mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika,

Mwenyekiti wa sasa Moussa Faki Mahamat ndie mgombea pekee wa nafasi hiyo.

Katika kiko cha leo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inatazamiwa kuchukua uwenyekiti kutoka kwa Afrika Kusini na itahudumu katika nafasi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja.

Kikao hicho kinatazamiwa kujadili masuala muhimu ya usalama barani Afrika kama vile hali katika Ukanda wa Sahel, Libya, Sudan Kusini na Somalia. Aidha viongozi hao wanatazamiwa kujadili hatua ambazo nchi za Afrika zimechukua kukabiliana na janga la COVID-19.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya kikao cha kilele cha Umoja wa Afrika ni: "Sanaa, Utamaduni na Turathi: Mihimili ya Kujenga Afrika Tunayoitaka."

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana