Uchunguzi huo wa maoni wa Chuo Kikuu cha Maryland na taasisi ya Iran Poll uliotolewa Alkhamisi wiki hii umeonyesha kuwa, washiriki asilimia 67 ya watu wa Iran wanaamini kuwa, nchi hiyo inapaswa kupiga hatua kuelekea kwenye kujitosheleza na kwenye uchumi ngangari na wa kimapambano, na asilimia 29 wamesema Tehran inapaswa kufanya jitihada za kufanya biashara na nchi nyingine.
Asilimia 85 ya walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni wamesema kuwa, utendaji wa mfumo wa afya wa Iran katika kipindi cha maambukizi ya corona ni mzuri sana.
Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yanaonyesha kuwa, asilimia 70 ya Wairani wanaamini kuwa, Marekani inazuia kufikishwa bidhaa muhimu na misaada ya kibinadamu nchini Iran.
Asilimia 60 ya Wairani wanasema Marekani haitatekeleza majukumu yake hata kama itarejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, na 84 wanasema wanaichukia Marekani.
Wairani asilimia 69 wanaamini kuwa, Tehran haipaswi kufanya mazungumzo na Marekani kabla ya Washington kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kutekeleza kikamilifu makubaliano hayo.
Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni pia yanasema kuwa, asilimia 88 ya wananchi wa Iran wanaamini kuwa harakati na shughuli za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini (Sepah) katika eneo la Magharibi mwa Asia zinadhamini zaidi usalama wa Iran na kwamba takwimu hizo zinaonyesha ongezeko la asilimia 13 ikilinganishwa na takwimu za mwezi Mei mwaka 2019.
Post a Comment