Featured

    Featured Posts

WIZARA YA KILIMO, JKT WAINGIA MKATABA KUBORESHA ZAIDI SEKTA YA KILIMO

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali  Charles Mbuge (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,  Gerald Kusaya wakibadilisha hati baada ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kilimo wakati wa  hafla iliyofanyika Makao Makuu ya JKT, Wilaya ya Chamwino, Dodoma. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali  Charles Mbuge (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,  Gerald Kusaya  wakitiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika kilimo wakati wa  hafla iliyofanyika Makao Makuu ya JKT, Wilaya ya Chamwino, Dodoma.


Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge akielezea jinsi ushirikiano na Wizara Kilimo utakavyochochea sekta ya kilimo katika vikosi vya jeshi hilo.
Mkuu wa  Tawi la Utawala JKT ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kimkakati ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi wa JKT, Kanali Hassan Mabena, akitoa taarifa kabla ya kusainiwa mkataba wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo na Wizara ya Kilimo.
Ujumbe wa Wizara ya Kilimo (kulia) na Jeshi la kujenga Taifa ukiwa  kikao hicho 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya akizungumza kabla ya kuingia Makubaliano ya Mkataba na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wa ushirikiano katika kuboresha Sekta ya kilimo katika hafla iliyofanyika Leo Februari 26,2021 katika Makao Makuu ya JKT, Wilayani  Chamwino, Dodoma.
Kusaya akifafanua jambo katika kikao hicho cha kusaini makubaliano hayo.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge (kulia) akimzawadia kalenda ya mwaka huu Katibu Mkuu wa Kilimo, Gerald Kusaya. Pamoja na ujumbe wake walikabidhiwa zawadi mbalimbali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,  Kusaya na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Mbuge  wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa jeshi hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,  Kusaya na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Mbuge wakiwa na maofisa wa wizara ya kilimo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,  Kusaya na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Mbuge wakiwa na maofisa wa jeshi hilo.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo akipanda mti katika viunga vya jeshi hilo ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu.Mkataba JKT na Wizara ya Kilimo Kupaisha Sekta ya Kilimo.

Na Richard Mwaikenda, Dodoma


Wizara ya Kilimo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) zimeingia mkataba wa ushirikiano katika sekta ya kilimo ili kuzalisha kwa tija kwa lengo la kuliwezesha Taifa kuwa na ziada ya chakula na mazao ya biashara.


Mkataba huo umesainiwa kwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara  ya Kilimo, Gerald  Kusaya   na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Mbuge leo Februari 26, 2021 katika makao makuu ya JKT wilayani Chamwino, mkoani Dodoma.


Akizungumza kabla ya kutiliana sahihi mkataba huo, Katibu Mkuu wa Kilimo, Kusaya amesema kuwa makubaliano hayo ni ya miaka mitano na kutaja baadhi ya maeneo ya ushirikiano kuwa ni; kuimarisha teknolojia bora za uzalishaji zinazoendana na wakati, Kujenga uwezo wa kusambaza teknolojia za kilimo, Huduma za umwagiliaji, Utafutaji masoko, huduma za usimamizi wa mazao pamoja na kuongeza thamani mazao yanayozalishwa na jeshi hilo.


Kusaya amesema kuwa si kwamba  ushirikiano na JKT ndiyo umeaanza siku hiyo, la hasha,  bali wameamua kuuboresha zaidi kwa lengo la kuleta tija zaidi katika uzalishaji wa mazao kwa vile wameona jitihada kubwa zinazofanywa na jeshi hilo kukuza sekta ya kilimo.


"Makubaliano haya yatawezesha Wizara ya Kilimo na Jeshi la Kujenga Taifa  kufanya tafiti za pamoja, kuanzisha mpango wa pamoja wa usambazaji wa taarifa za kilimo ikiwemo teknolojia, kubadilishana taarifa za masoko, kufanya usimamizi na tathmini ya pamoja," amesema Kusaya.


Naye, Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Mbuge akizungumza katika hafla hiyo, amesema kuwa makubaliano hayo yamekuja wakati muafaka kwani vijana wengi wa Tanzania wamekuwa wakijitolea kwenye mafunzo ya JKT na kwamba wakiwa ndani ya JKT watapatiwa mafunzo ya Kilimo ambapo wana uhakika na wao wataenda kuitumia vizuri pindi watakaporejea  uraiani. 


"Jeshi hili ni chombo pekee ambacho kikitumika  katika kukuza sekta ya kilimo kitaleta matokeo makubwa katika sekta ya kilimo naahidi kuendelea kushirikiana na Wizara ya Kilimo ili kuhakikisha kuwa malengo yaliyopangwa yanafikiwa," amesema Meja Jenerali Mbuge.


Aidha, Meja Jenerali Mbuge amesema JKT katika mwaka 2019/ 2020 na 2020/2021 imeanzisha kilimo cha kimkakati katika maeneo mbalimbali ikiwemo kupitia kikosi cha Chita wilayani Kilombero mkoani  Morogoro ambapo inazalisha mpunga kwenye eneo la ekari 2500 na baadae ekari 12,500 na kwamba lengo ni kuongeza uzalishaji mara dufu.


Meja  Jenerali  Charles  Mbuge alimalizia kwa kwa kuupongeza ushirikiano uliopo kati ya JKT na Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ikiwemo Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) na ASA.


Kwa upande wake,  Mkuu wa Tawi la Utawala JKT ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi  JKT Kanali Hassan Mabena amesema kuwa wamechukua hatua za makusudi katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili kutimiza azma ya Taifa kujitegemea kwa chakula na pia kuzalisha mazao ya biashara.


Amesema kuwa katika kuimarisha uzalishaji JKT imenunua matrekta 15 pamoja na zana nyingine za kilimo kwa lengo la kuzalisha kwa tija.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana