Na Mwandishi wetu
Waumini wa Kanisa la Baptist Omurushaka wilayani Karagwe Mkoani Kagera wamemuomba Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli kuunda tume ya kuchunguza mgogoro wa ardhi wa kiwanja no 100 kitalu D Mali ya Kanisa hilo eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya shule ya msingi bohari inayofanya vizuri wilayani humo baada ya Kanisa hilo kushinda kesi Mara kadhaa bila kupata muafa tangu mwaka 2003.
Wakizungumzia Hali hiyo waumini wa Kanisa hilo akiwemo Nelson Wilson, Pius Beichumila Clementina Deus na Speratu Tshema wamesema mgogoro ulioanza mwaka 2003 ni Kati ya mshitaki / mdai aliyetajwa kwa jina Ally Chamani ambaye pia ni mwanasheria wa mahakama kuu ya Bukoba Mkoani Kagera na Kanisa la Baptist mgogoro ambao wamedai kuwa licha ya kushinda kesi kadhaa hauonyeshi mafanikio na umesababisha kuathili huduma ya Kanisa pamoja na shule kwani wanafunzi upata Elimu kwa wasi wasi hivyo kumuomba Rais Magufuli kuingilia Kati ili huduma ya jamii iendelee.
Akizungumzia Hali hiyo mchungaji wa Kanisa la Baptist Omurushaka Karagwe Dioniz Karwani amesema kuwa katika kesi hiyo no 3 ya mwaka 2003 mdai alimshtaki mkurugenzi wa wilaya ya Karagwe pamoja na Kanisa hilo ambapo aliipeleka mahakama ya wilaya ya Karagwe na baadaye kushindwa kesi hiyo.
Amesema kuwa 2003 muhusika hakuishia hapo alikata rufaa katika mahakama kuu ya Bukoba kesi no 15 ya mwaka 2006 chini ya Jaji PB Khaday ambapo pia alishindwa.
Karwani ameongeza kuwa baada ya mshitaki kushindwa aliamua kufungua kesi hiyo kwa Mara nyingine katika mahakama kuu ya Bukoba kesi no 29 ya mwaka 2014 chini ya Jaji SB Bongole J na kushindwa Kisha kudai kulipa madai ambayo aliikatia rufaa kukataa gharama za kesi hiyo nayo akashindwa, na kuamua kufungua kesi katika mahakama kuu ya Bukoba yenye namba 6 ya mwaka 2018 chini ya Jaji N.N Kilekamajenga na pia kushindwa.
Mchungaji Karwani amesema kuwa mdai huyo ambaye ni mwanasheria aliamua kufungua tena kesi no 60 ya mwaka 2016 na kushindwa na kuwa 2021 amefungua kesi no 3 na kesi no 67 ya mwaka 2020 ambazo ziko mahakama kuu ya Bukoba.
Mchungaji wa Kanisa hilo na meneja wa shule ya msingi bohari iliyojengwa katika kiwanja hicho chenye mgogoro amesema kwa anachokiomba kwa Rais Magufuli ni kuchunguza mgogoro kwa kuundwa tume itakayosaidia mgogoro huo kuisha .
" Vibali vyote vipo Kanisa limelipia hata stakabadhi za kiwanja hicho miaka yote na kiwanja kilinunuliwa na kimeisha pata ofa hapa uwenda Kuna rushwa na uzembe Rais wetu ni msikivu mpenda maendeleo atatusaidia" alisema mchungaji Karwani
Aidha ameongeza kuwa Kanisa kwa kuwa lilitaka maendeleo lilifanya mabadiliko kwa waziri mwaka 2005 kuwa matumizi ya kiwanja kwa matumizi ya shule ambapo pia tume kutoka halmashauri ya wilaya ya Karagwe iliundwa ili kufuatikia kiwanja hicho na kulidhia kuwa kiwanja hicho ni Mali ya Kanisa ambapo wahusika waliandaliwa barua juu ya kujenga isivyo halali katika kiwanja No 100 kitalu D.
Hata hivyo kwa upande wake mshitaki Ally Chamani (mwanasheria)akiongea na blog ya taifa kwa njia ya simu amesema kuwa kesi hiyo inaendelea mahakamani ambapo amedai kuwa mwanzoni alifungua kesi hiyo lakini alishtaki kisheria mtu ambaye hayupo duniani .
Post a Comment