Maria akiingiza taarifa za mteja kwenye mfumo wa kidijitali
Mrumah akimpatia maelekezo mmoja wa wateja wapya.
Maria akimpiga picha mmoja wa wateja wapya
Mteja mpya akiweka alama za vidole
Wateja wakipata huduma ya kibenki
Mteja akipata maelezo ya jinsi ya kujiunga na benki hiyo.
Mteja akiweka alama ya kidole kwenye mfumo wa kidijitali.
Na Richard Mwaikenda, Chamwino.
BENKI ya NMB Tawi la Chamwino, mkoani Dodoma, limepata wateja wengi wa papo kwa papo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wa miwa na alizeti yaliyoendeshwa na Mpango wa Urasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) katika Kijiji cha Manyemba, Kata ya Dabalo wilayani humo.
Wengi walihamasika kujiunga na benki hiyo baada ya kuelimishwa na Afisa Uhusiano na Mikopo wa Benki hiyo Tawi la Chamwino, Emil Mrumah kuhusu umuhimu wa kuweka fedha benki na faida zake. Zaidi ya wakulima 70 walihudhuria mafunzo hayo.
Mrumah aliwaeleza kuwa mkopo kwa ajili ya kilimo una riba nafuu ambapo wanaweza kukopeshwa trekta JIPYA la Sh.milioni 40 kwa kulipa asilimia 20 tu na kukabidhiwa na deni hulipwa ndani ya miaka mitano. Pia mkulima hupangiwa kulipa deni kila baada ya mauzo ya mazao yao.
"Wakulima changamkieni fursa hiyo, jiungeni na NMB upate mkopo wa trekta mpya, sifa za mteja ni kuwa na shamba hata likiwa la kukodi, kubwa ni kuwa na rekodi ya kuvuna mazao kwa faida," alisema Mrumah.
Siku hiyo zaidi ya wananchi 23 walijiunga na NMB na kupatiwa kadi zao na wengi wao kuahidi kesho yake kwenda kujiunga kwani siku hiyo walikuwa hawajajiandaa. Zaidi ya wakulima 40 waliahidi kujiunga na kwenda kuwahamasisha wengine.
Wakulima hao ambao NMB imeingia nao mkataba wa kutengeneza miondombinu ya kilimo cha miwa, walipata pia mafunzo ya jinsi ya kuandaa shamba la miwa, kupanda kwa kufuata mistari na nafasi, mbolea zinazofaa kudhibiti wadudu waharibifu, parizi na hatimaye kuvuna mazao bora.
Pia, walifundishwa jinsi ya kuweka kumbukumbu za mradi wa kilimo hicho, kupanga mpango wa biashara, faida ya kumilikisha ardhi na hati kuzitumia kama dhamana kukopa fedha benki,kuthaminisha mali na kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo ya kilimo cha miwa na alizeti.
Katika Kijiji hicho panatarajiwa kujengwa kiwanda cha sukari ambapo miwa ya kutengenezea sukari itakuwa inanunuliwa kutoka kwa wakulima watakaokuwa wameingia nao mkataba.
Post a Comment