Kwa mujibu wa habari hizo, gari lililokuwa limebeba Waandishi wa habri katika msafara huo limepinduka mara nne na kusababisha majeruhi.
Inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni gari moja aina ya Escudo lenye rangi nyeupe lililokuwa likiendeshwa na mzungu mmoja baada ya kupita msafara wa polisi na Makamu wa Pili wa Rais lilichomoka na kutaka kuendelea na safari wakati msafara wote haujamalizika.
Kwa mujibu wa habari hizo baada ya hapo dereva wa gari lenye waandishi alihofia kugongana uso kwa uso na gari hilo la mzungu akaamua kwenda pembeni hatua iliyofanya gari kupinduka na kwamba baadhi ya majeruhi ambao idadi yao haijatajwa wamepelekwa haraka Hospitali ya Makunduchi ambako wamelazwa.
Post a Comment