Na Mwandishi Maalum
Diwani wa Kata ya Msasani, Kionondoni, Jijini Dar es Salaam, Luca Neghest, amesema dhamira yake ni kuona wananchi wa Kata hiyo hasa wanaoishi katika Mitaa ya Mikoroshini na Bonde la Mpunga wanaondokana na changamoto kubwa ubovu wa za miundo mbinu hususan barabara na mitaro.
Luca amesema katika kufanikisha hilo tayari amepata Mkandarasi Kampuni ya Nzinga Constructions and Plumbering Limited ambaye ameanza kufumua kabisa mitaa hiyo ili kujenga miundombinu ya kisasa hasa ya mifereji na mitaro katika barabara.
Anaeleza ujenzi huo unagharimu zaidi ya sh. milioni 10 ambazo anagharimia zikiwa ni fedha zake mfukoni.
“Najitolea kwa nguvu zangu mwenyewe kwa sababu wananchi katika mitaa hii wameishi kwa adha kubwa iliyo watesa kwa kipindi kirefu,”anaeleza Diwani Luca.
Anasema, baada ya kuona adha ya mafuriko waliyokuwa wakiipata wananchi wa Msasani hususan Bonde la Mpunga na Mikoroshoni, aliamua kumtafuta mkandarasi mzalendo Nzinga ili kuona namna gani watashirikiana kuwaokoa wananchi.
“Nashukuru Nzinga walikubari kutusaidia hivyo ujenzi huu wa mifereji, kuweka makavati katika maeneo korofi ni wa kujitolea na gharama yake ni zaidi y ash. milioni 10 ambazo nimegharamia, anaeleza diwani huyo.
Anasema maendeleo katika kata hiyo si kwa mitaa hiyo bali Kata nzima ya Msasani inayohusisha pia mitaa ya Masaki na Oysterbay.
“Tumeanza na mitaa ya Mikoroshoni na Bonde la Mpunga, lakini nitagusa maeneo yote ya Kata ya Msasani ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto,” ameeleza Diwani huyo.
Mhandisi wa Kampuni ya Nzunda , Jordan Mbaga, alisema kazi ya kuweka makarabati inaendelea kwa kasi na imefikia asilimia 12.
“Dhamira ni kudhibiti maji yasiingie katika nyumba za watu bali yafuate mkondo.Tutajenga mfereji hadi Bahari ya Hindi,”ameeleza Mhandisi Mbaga.
Post a Comment