Featured

    Featured Posts

DC MHELUKA AKABIDHI VIFAA VYA UJENZI WA MRADI WA UMEME WA REA KWA KAMPUNI YA NAKUROI INVESTMENT CO. LTD, VILIVYOKUWA VIMEIBWA

 Angela Sebastian, Bukoba 

Mahakama ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera imekabidhi kampuni ya ukandarasi wa kujenga line za umeme Vijijini ya Nakuroi Investment co. ltd vifaa vya ujenzi wa mradi wa umeme Vijijini hawamu ya tatu mzunguko wa kwanza (Rea),vyenye thamani ya shilingi milioni 73 ambavyo vilikuwa vimeibiwa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu mwaka 2019.


Mwendesha mashitaka wa Serikali Adropha Maganda akiongea baada ya makabidhiano hayo yaliyofanyika kati ya hakimu wa mkazi mwandamizi waWilaya hiyo Frola Haule na mkuu wa Wilaya hiyo Godfrey Mheluka na baadaye kwa   kampuni ya Nakuroi ambayo inaendelea na ujenzi wa mradi huo, alisema vifaa hivyo viliibiwa katika ghara la kampuni hiyo lililoko Kijiji cha Kishao kata Bugene Wilayani Karagwe.


Maganda amesema tukio hilo lilitokea mwaka 2019 ambapo gari aina ya canter namba T 370 DHH likiwa limepakia vifaa hivyo na ikielekea kusikojulikana ambapo raia wema walitoa taarifa kwa uongozi wa kampuni ya Nakuroi nao walitoa taarifa polisi na kufanikisha kulikamata gari hilo na watuhumiwa watu.


"Kesi namba 327 ya mwaka 2020 ya wizi iliendelea na hukumu imetolewa Aprili ,14 mwaka huu ambapo, watuhumiwa watatu walikamatwa mmoja ametiwa hatiani na kufungwa miaka mitano huku wawili kuachiwa huru pamoja na gari limekabidhiwa kwa mwenye nalo"ameeleza Maganda


Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Juma Abdalah mfanyabiashara aliyehukumiwa kufungwa jera miaka mitano,Godlesten Lema aliyekuwa dreva na Hussein Sadick aliyekuwa kondakta wa gari lilolokuwa limebeba mzigo huo wa wizi ambao hawakupatikana na hati na mahakama imewaachia huru.


Naye hakimu mkazi mwandamizi wa Wilaya hiyo Frola Haule wakati akikabidhi vifaa hivyo amesema kilichofanyika leo ilikuwaa ni utekelezaji wa mahaka baada ya hukumu aliyoitoa Aprili 14 mwaka huu  iliyokuwa inahusu  kesi ya wizi kifunfu cha 258 na 265 Cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya16 ya 2002.


Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Serikali Mkuu wa Wilaya hiyo Godfrey Mheluka amesema mali hiyo yenye thamani ya shilingi  milioni 73 zimekabidhiwa mikononi mwa kampuni ya

 Nakuroi investment co.ltd kwani mali hizo zinarejeshwa kwa ajili ya kwenda kutekeleza miradi ya umeme ambayo itanufaisha wananchi kama ilivyolengwa na Serikali.


"Wananchi mnakumbuka mwaka 2019 kuna vifaa vya Rea ambavyo vilikuwa vinatumika kujenga line za umeme katika Wilaya hii,kwa ushirikiano wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama tulifanikiwa kuvikamata na sasa vimekabidhiwa,nawashauri vyombo ulinzi na usalama kuendeleza ushirikiano katika kulinda mali za Umma na wananchi na kutenda haki maana palipo na haki amani inatamalaki"ameeleza Mheluka.


Naye Afisa manunuzi kutoka kampuni ya Nakuroi makao makuu iliyokuwa inajenga mradi huo,Abraham Laizer amesema tangu wameanza mradi katika mkoa wa Kagera wizi kama huo umekuwa ukitokea katika maeneo mbalimba ya mkoa huu hivyo, kuchangia kurudisha nyuma maendeleo ya mradi na kusababisha kutokamilika kwa wakati ingawa wamekuwa wakijitahidi kuona wanafikia malengo ya Serikali.


Nao baadhi ya wananchi waliokuwepo maeneo ya kotuo cha polisi cha Kayanga Wilayani Karagwe ambao mahakama ilihamishia shuhuli zake kwa muda wamesema watu wanaohujumu vifaa kama hivyo wachukuliwe hatua kali ikiwemo kufungwa jera.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Gofrey Mheluka akikabidhi vifaa vya kujenga mradi wa umeme Vijijini REA kwa uongozi wa Kampuni ya Nakuroi investment co. Ltd vyenye thamani ya Sh. milioni 73, baada ya kukabidhiwa na Mahakama ya Wilaya hiyo vilivyokuwa vimeibwa. (Picha na Angela Sebastian).
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana