Mkurugenzi wa Kampuni ya Bravo Agency Abbasi Mtemvu, ametoa msaada wachakula kwa watu wenye ulemavu, ili kiwasaidie katika Mwezi Mtufuku wa Ramadhani.
Mbunge huyo wa zamani wa Jimbo la Temeke, amekabidhi msaada huo leo, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni kawaida yake kila inapofika mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa makumdi mbalimbali ya watu wenye uhitaji maalumu.
Chakula hicho kinahusisha unga wa ngano, sembe, sukari, mafuta ya kupikia na tende.
Akikabidhi msaada huo, Mtemvu alisema amekuwa akitoa msaada kila ifikapo mwezi Mtukufu wa Ramadhani na wakati wa Sikukuu za Krismas ili kuisaidia jamii yenye mahitaji maalumu.
"Hii imekuwa ni kawaida yangu kutoa sadaka.Tangu nikiwa Mbunge wa Jimbo la Temeke na sasa sio Mbunge lakini naendelea kutoa kila ikifika wakati huu na Krismass," alisema Mtemvu.
Alisema pia ataendelea kutoa msaada kwa vituo vya watoto yatima ili kuwapa mahitaji muhimu hususan chakula.
Alisema ni vizuri kuwasaidia watu hawa wenye mahihitaji maalumu ili na wao wajione sehemu ya jamii, watu wenye uwezo wa kutoa msaada na wao wakasaidia watu hao.
Post a Comment