Mbunge Masache Kasaka wa Chunya jimbo ambalo ni miongoni mwa vinara kwa machimbo ya almasi na dhahabu nchini, ameishauri Serikali kufungua Chunya ofisi za Taasisi ya Jiolojia (GST), inayofanya utafiti wa madini nchini ili kuwapunguzia usumbufu wachimbaji madini kusafiri hadi Dodoma ilipo GST kupima viwango vya madini kwenye udongo.
Akichangia majadiliano ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mbunge Kasaka, amesema Serikali ikitekeleza ombi hilo, licha kuwaondolea usumbufu wachimbaji, pia serikali itaongeza wigo wa mapato kutokana na kodi itakayotozwa kupitia kwenye madini yenye ubora ambayo kiwango chake kitaongezeka kutokana na majibu ya haraka ya utafifiti utakaokuwa unatolewa...
Post a Comment