Featured

    Featured Posts

HALI YA MAMA JANETI MAGUFULI SIYO NZURI KIAFYA KUTOKANA NA MSTUKO ALIOPATA KUFUATIA KIFO CHA MUMEWE DK. MGUFULI

Joseph Magufuli, mtoto wa Hayati Dk. John Magufuli akizungumza kwenye Kongamano la Viongozi wa Dini kumuombea aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dk. John Magufuli lililofanyika katika Ukumbi wa Chimwaga, Dodoma, leo


CCM Blog, Dodoma

Joseph Maguli, mtoto wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dk.John Magufuli, amesema mama yake, Janeth Magufuli hayupo vizuri kiafya kutokana na mshtuko aliopata kufuatia kifo cha mumewe kilichotokea Machi 17, 2021 jijini Dar es Salaam.


Akizungumza leo Aprili 18, 2021 katika Kongamano la Viongozi wa Dini kumuombea aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dk. John Magufuli lililofanyika katika Ukumbi wa Chimwaga, Dodoma, mgeni rasmi, Rais Samia Suluhu Hassan Joseph amesema, Mama Janeti Magufuli bado anaendelea na matibabu.


“Mama hakuweza kuja kwa sababu ya tatizo la kiafya alipatwa na mshtuko baada ya baba kufariki, yupo anaendelea na matibabu, mama anawashukuru viongozi wa dini na watu wote kwa kuliombea Taifa wakati wote wa msiba.


Na hakika ilikuwa jambo gumu kumpoteza mzazi na kiongozi wa Taifa, "ameeleza Joseph wakati akizungumza kwenye Kongamano la Viongozi wa Dini lililofanyika leo mjini Dodoma.


Pia mtoto huyo wa Hayati Magufuli, ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kumuomba Mungu ili upendo, amani na mshikamano viendelee kutawala nchini.


Joseph amewashukuru viongozi wa dini na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wote nchini ambao walikuwa pamoja nao tangu walipompoteza baba yao hadi maziko.


Awali Mufti wa Zanzibar, Sheikh Al Kaabi, amewataka Watanzania kuwa na utii kwa viongozi kwa kuwa wamepata bahati ya kuwa na viongozi wenye nia njema kwa ajili ya kuliongoza Taifa.


Sheikh Al Kaabi akiwasilisha mada ya utii na uzalendo kwa umoja wa Taifa, amesema ni muhimu kila mmoja ampe haki mwenzake bila kutanguliza tofauti za kidini, itikadi na ukabila.


“Ni wajibu wetu kuwatii viongozi bila kujali ukubwa wala udogo wao. Tuna bahati nzuri tumepata viongozi wenye nia nzuri na makusudio mema kwetu na Tanzania nzima.

 

Nikimzungumzia mama Samia (Rais Samia Suluhu Hassan) ni kiongozi wa kwanza mwanamke, mwanamke ni mtu mwenye huruma na tunaamini mama Samia una huruma kwa wananchi wako", alisema Sheikh Al Kaabi.


Kwa upande wake, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amesema Hayati Dk. John Magufuli alikuwa na utu, alijenga uadilifu, uaminifu kwa watendaji na wafanyakazi na alikemea maovu kwa maslahi mapana ya Taifa.


“Mafunzo mengine aliyotuachia ni utu, alikuwa akiwajali watu, kuwasaidia wanyonge kupata haki zao, kuwaonea huruma lakini pia alikuwa na ukarimu kwa watu, kubwa sana na ambalo nimeona wasaidizi wake wakilifanya ni kujishusha ambayo ni silaha kubwa sana kwa nafasi uliyonayo.


Pia alikuwa mstari wa mbele kutatua matatizo ya watu yaliyobana akayapa ufumbuzi, kujenga nidhamu yeye na aliyekuwa makamu wake wa rais na waziri mkuu walifanya kazi kubwa sana ya kutatua matatizo makubwa ya nchi,” amesema Muft.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana