Featured

    Featured Posts

RAIS SAMIA NA RAIS DK. MWINYI WAHUDHURIA KONGAMANO LA KUMUOMBEA DUA RAIS WA AWMU YA TANO HAYATI JOHN MAGUFULI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali akishiriki kuomba dua kabla ya kuanza kwa Kongamano la Viongozi wa Dini la Kumuombea na Kuombea Taifa pamoja na kumshukuru Mungu kwa ajili ya Maisha ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma leo Jumapili Aprili 18, 2021.

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Zubeiry akiendesha mada wakati wa kongamano hilo.
Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi akizhutubia wakati wa kongamano hilo.

Wananchi wakiungana na viongozi wa Dini kuomba dua
Baadhi ya wanafunzi wakiomba dua

Viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma wakiungana na viongozi wengine kumuombea dua Hayati John Magufuli



Wananchi wakifurahia moja ya mada iliyotolewa na viongozi wa dini wakati wa kongamano hilo

Azim Dewji akitoa mada wakti wa kongamano hilo
Sehemu ya umati ukishiriki kwenye kongamano hilo





Mkuu wa Dayosisi ya  Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Alex Malasusa (kushoto), akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rodrick Mpogolo na Msajiri wa Vyma vya Siasa. Askofu Malasusa  alikuwa muongozaji wa kongamano hilo.


Rais Samia Suluhu Hasan akihutubia wakati wa kongamano hilo ambapo aliwashukuru viongozi wa Dini kwa kuandaa Kngamano hilo la kumuombea Rais wa Awamu ya Tano Hayati John Magufuli.Picha zote na Richard Mwaikenda
Mtoto mkubwa wa Hayati John Magufuli, Joseph akitoa shukrani kwa viongozi wa dini kuandaa kongamano hilo l kumuombea dua baba yake, lakini pia alitoa shukrani kwa viongozi wa juu na watanzania kwa ujumla walivyoshiriki kwenye kongamano hilo pamoja na mazishi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana