Mada zilizowasilishwa ni; Historia ya Muungano na Farsafa tofauti za aia mbalimbali za muungano wa kisiasa duniani. Faida za kiuchumi, kijamii na kisiasa zitokanazo na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Baadhi ya washiriki
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Seleman Jaffo akizungumza wakati wa kuanza kwa kongamano hilo.
Mwongoza Mjdala wa Kongamano ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante ole Gabriel akielezea kuhusu utaratibu na lengo la kongamano hilo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mchokoza mada Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi akielezea kuhusu histori ya Muungano na sababu za kuufanya udumu hadi sasa.
Mwanasiasa mkongwe aliyewahi kuwa Rais na Mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, Balozi Getrude Mongella akielezea ndoto yake ilivyotimia ya Tanzania kuongozwa na Mwanamke, Samia Suluhu Hassan na kwamba anaiweza kazi kinachotakiwa ni kumuunga mkono.
Baadhi ya mawaziri wakiwa kwenye kongamano hilo
Mbunge kupitia kundi la vijana Tanzania kutoka Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, Latifa Khamis Juakali akielezea umuhimu wa vijana kuudumisha Muungano.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, Shibuda akiwa miongoni mwa wanasiasa waliohudhuria kongamano hilo
Mwenyekiti wa Viongoziwa Madhehebu ya Dini Mkoa wa Dodoma, ambaye ni Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajab Shabani akichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Meya wa Jiji la Dodoma, Davis Mwamfupe akichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, akitoa neno la shukrani na kufunga kongamano hilo.
Post a Comment