Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga akisaini kwenye kitabu cha rambirambi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa, Jackson Kiswaga akitoa salamu za rambirambi za kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dk. John Magufuli ambapo amemmwagia sifa lukuki zikiwemo za uchapakazi wake, uzalendo kwa nchi yake kiasi cha kuiletea nchi maendeleo kwa kipindi kifupi cha miaka mitano ambapo pia alielezea imani yake kwa Rais mpya Mama Samia kwa kwa naye ni mzalendo na alifanya kazi kwa karibu na Magufuli atakamilisha miradi yote waliyoianzisha kwa kufuata Ilani ya CCM..Mdau nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video Mbunge Kiswaga akielezea jinsi alivyoguswa na msiba huo mkubwa kwa Taifa....Imeandaliwa na Richard Mwaikenda Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 0754264203
Post a Comment