RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Abeid Amani Karume wakati wa kisomo cha kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo kilichofanyika leo Mjini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiongoza kisoma cha Dua na Hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume, iliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Waziri Mkuu wa Tanzania Alhajj Kassim Majaliwa na (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi.
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha hitma ikisomwa na Bi.Maryam Mliwa (kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Mama Zuhura Kassim na (kulia kwa Rais) Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Sharifa Omar Khalfan. Wakiitikia dua.
MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akisoma dua baada ya kumalizika kwa kisomo cha hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume n a (kushoto kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi na (kulia) Waziri Mkuu wa Tanzania Alhajj Kassim Majaliwa
Post a Comment