Featured

    Featured Posts

RAIS SAMIA ACHAGULIWA KWA KISHINDO KUWA MWENYEKITI WA CCM, AAHIDI KUSIMAMIA KWA DHATI MAMBO YATAKAYOZIDI KUKIPAISHA CHAMA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Dodoma

Rais Samia Suluhu Hassan, amechaguliwa kwa kishindo kuwa Mwenyekiti wa sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, leo.


Akitamgaza matokeo ya Uchaguzi huo, Spika wa Bunge Job Ndugai alisema, Samia amepitishwa kuwa Mwenyekiti baada ya kupata kura 1862 sawa na asilimia 100 ya kura zote 1862 zilizopigwa na Wajumbe  katika Mkutano huo mabo umeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Mzee Philip Mangula.


"Wajumbe wa mkutano huu ni 1876, kura zilizopigwa ni 1862, matokeo ni kwamba Rais Samia amepata jumla ya kura 862  sawa na asilimai 100, hakuna kura iliyoharibina wala ya hapana", akasema Spika Ndugai.


Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti mpya, Mama Samia amesema licha ya kufahamu kazi aliyokabidhiwa siyo nyepesi lakini anaamini kwa uzoefu alionao anatosha na anaweza kuifanya kwa weledi na uwezo mkubwa.


Mama Samia amesema kwa miaka 20 ya kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM anafahamu kuwa changamoto zinazowakabili watendaji wa ngazi za Mikoa na Wilaya ikiwemo ya usafiri ambapo ameahidi kuyatatua kwa kushirikiana na wanachama wa CCM.


"Ninafahamu kuna changamoto za uhaba wa vitendea kazi kama usafiri kwenye Wilaya zetu na Mikoa yetu jambo ambalo linalofifisha utendaji kazi wa kukijenga chama chetu na Nchi yetu kwa ujumla.


Changamoto nyingine ni maslahi duni kwa watendaji wetu pamoja na malimbikizo ya madai ya stahiki ikiwemo ya uhamisho na kustaafu, niwaahidi nitashirikiana nanyi katika kutatua changamoto hizo kwa pamoja, " Amesema Rais Samia.


Rais Samia pia amesisitiza kusimamia maadili, kanuni na taratibu za chama hicho ili kuweza kufanya kazi kwa weledi katika kuwatumikia watanzania na wanachama wa CCM.


Kadhalika pamoja na Uchaguzi huo wa Mwenyekiti wa CCM, umefanyika pia Uchaguzi wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM ambapo matokeo yake yalitangazwa Spika wa Baraza la Wawakilishi.


Katika matokeo ya Uchaguzi huo zilikuwa kura1839, zikaharibika 16, halali 1823 na katika kinyang'anyiro 

Kulwa Bululu alipata kura 403,  Asha Sadru (434), Nduvu Chengula (542), Fadhili Salum (577), Happy Mgongo (839), Rehema Simba (867) na walioshinda ni Hapiness Mgongo na Rehema Simba.


Katika mkutano huu pia imeshuhudiwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Lazaro Nyalandu akitangaza kukihama chake na kurejea CCM.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana