Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Ddodoma
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, amethibitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Dk. Abdallah Juma Saadala kuendelea na nafasi hiyo.
Katika Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, chini ya Mwenyekiti wa Sita wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, NEC imewathibisha Wajumbe wapya wa Sekretarieti ya NEC ya CCM, katika kushika nafasi mbalimbali ambapo
Wajumbe hao wa NEC ya CCM ni Shaka Hamdu Shaka ambaye anakuwa Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi ambaye amechukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Humphrey Polepole ambaye sasa ni Mbunge wa Kuteuliwa.
Wengine ni, Katibu wa NEC Idara ya Uchumi na Fedha Dk.Frank George Hawasi ambaye anaendelea na wadhifa huo, Katibu wa NEC Oganaizesheni Maurdin Kastiko ambaye amechukua nafasi iliyokuwa chini ya Pereira Ame Silima na Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga ameendelea na nafasi yake ya Katibu wa NEC, Idara ya Siasa na mambo ya Nje. Wote hao wamethibitisha na NEC baada ya majina yao kupendelekezwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Samia a Mapinduzi (CCM) Rais Samia Suluhu Hassan.
Akitangaza mapendekezo hayo Mwenyekiti Rais Samia alisema, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo na Pereira Ame Silima aliyekuwa Katibu wa NEC Oganaizesheni watapangiwa majukumu mengine.
Post a Comment