NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta ameridhishwa na ukusanyaji wa mapato katika kituo cha foroza Cha Namanga kilichopo wilaya Longido kwa mwezi Machi ambao umevuka lengo la billioni 5.3 na kufikia billioni 7.1.
Kimanta aliyasema hayo wakati alipotembelea kituo cha mpaka huo wa Tanzania na Kenya katika ziara yake ya kawaida yenye lengo la kuona utendaji kazi wa mpaka ambapo alisema kuwa ameridhishwa na ukusanyaji wa mapato kwa namna yalivyopanda.
“Lengo ni kuona utendaji kazi, hali ya upitishaji na uingiaji wa mizigo lakini tumeona kuwa mapato yamepanda kwa mwezi Machi hili ni jambo zuri na jema na shukrani ziende kwa serikali ya Tanzania na Kenya kwa kukubali kujenga kituo hiki Cha pamoja,” Alisema Kimanta.
Aidha kuhusiana na suala la usafirishaji waahindi kwenda nchi ya Kenya, Kimanta alieleza kuwa bado serikali ya Kenya haijaruhusu mahindi ya Tanzania kuingia katika nchi yao lakini wafanyabiashara wameshauriwa kutafuta masoko ya ndani ndio maana magari ya mahindi yaliyokuwa yakisubiria kuingia Kenya hayapo.
“Kama mnavyoona magari ya mahindi hayapo, tuliwashauri wafanyabiashara kuuza mahindi kwenye masoko ya ndani na wamefanya hivyo na wamefanikiwa kwani ndani ya nchi yetu bado Kuna soko kubwa la mahindi kulingana na uhitaji wa wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu,” Alieleza.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe alisema kuwa Kama wilaya wanatoa shukrani kubwa kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta ambaye amekuwa akiwapa ushirikiano mkubwa jambo limalochangia ufanisi wa kituo hicho hasa ukusanyaji wa mapato.
Kuhusiana na utoroshaji wa mifugo unaofanywa na baadhi ya watanzania Mwaisumbe alisema kuwa wametembelea minada nchini Kenya kwenye wilayani za jirani na mpaka huo ikiwemo Kajado na Usriver ambapo wameweza kuzungumza na wasimamizi wa minada hiyo ilikiweza kutoa taarifa za mifugo iliyotoroshwa kwani wanajua mifugo iliyolipiea Kodi na ambayo haijalipiea.
“Tumekubaliana kuwa na vikao kila baada ya miezi mitatu kwani tumekuta mifugo iliyotoroshwa na Kuna baadhi ya watu waliohusika wamejidalimisha na wametueleza mbinu na njia zote wanazozitumia kutorosha na tumeanza kuzifanyaia kazi,” Alieleza Mwaisumbe
“Hatuatashughulika na mifugo peke yake bali na magendo mengine ambayo yanafanyika kwani mpaka wetu ni mkubwa una kilometa 323 ambapo Kuna baadhi ya watanzania ambao sio waaminifu, wanakwepa kulipa kodi na tumeanza kuwakamata na pia tunaanda ripoti kwaajili ya kupeleka ofisi ya mkoa,” Alifafanua.
Naye Meneja msaidizi wa foroza mkoa wa Arusha Paul Kamukolu alieleza kuwa wamevuka lengo kwa asilimia 131 tofauti na miezi mingine ambapo walikuwa wakikusanya sawa na lengo au chini ya lengo lakini hivi sasa wamevuka na kukusanya billion 7.1 huku lengo likiwa ni billion 5.3.r
Post a Comment