*************************************
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU 24 KWA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI IKIWEMO MAUWAJI NA KUVUNJA OSIFI ZA SHULE ZA MSINGI NA KUIBA VITABU.
TUKIO LA KWANZA
KWA KIPINDI CHA MIEZI MIWILI (FEBRUARI NA MACHI) KWA NYAKATI TOFAUTI OFISI ZA SHULE TATU ZA MSINGI WILAYA YA KWIMBA, ZILIGUNDULIWA KUVUNJWA NA KUIBWA VITABU 529 VYA MITAALA MIPYA VYA MASOMO MBALIMBALI AMBAPO, WALIMU NA WALINZI WA SHULE HIZO WALIKULA NJAMA YA KUIBA VITABU NA KUTENGENEZA MATUKIO YA KUFIKIRIKA YA KUVUNJA ILI KUFICHA UHALISIA WA WIZI HUO . BAADA YA UPELELEZI WA KINA, JESHI LA POLISI LILIBAINI KUWA VITABU HIVYO VILIIBWA NA KUUZWA KWA WAFANYA BIASHARA WA MADUKA YA VITABU AMBAO BAADA YA MAHOJIANO YA KINA WALIKIRI KUHUSIKA NA UNUNUZI WA VITABU HIVYO. AIDHA, BAADHI YA VITABU VILIVOKAMATWA KWA WAUZA MADUKA HAO VIMEKUTWA VIMEFUTWA MAANDISHI YENYE KATAZO LA KUTOUZWA KWA MALI YA SERIKALI. MTUHUMIWA MENGI MUHETA, MIAKA 43, MWALIMU, SHULE YA MSINGI KISHIRI, NA WENZAKE 18 WANASHIKILIWA KWA MAHOJIANO YA KINA NA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO.
TUKIO LA PILI
WATU WAWILI MAJINA YAO YAMEHIFADHIWA KWA AJILI YA UPELELEZI WAMEKAMATWA KWA TUHUMA ZA KOSA LA MAUAJI YA MTU MMOJA MWANYE UMRI KATI YA MIAKA 40-42 YALIYOTOKEA ENEO LA KANYERERE, KATA YA MKUYUNI, WILAYA YA NYAMAGANA KWA KINACHODAIWA NI WIVU WA KIMAPENZI. AIDHA, KANDO YA MWILI WA MAREHEMU KULIKUTWA UJUMBE ULIOSOMEKA KUWA “MKE WA MTU NI SUMU”. WATUHUMIWA WANAFANYIWA MAHOJIANO YA KINA NA UPELELEZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO.
TUKIO LA TATU
LINAHUSU KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA SUGU ALIYE KUWA ANAJIHUSISHA NA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA AINA YA BHANGI ENEO LA BUSWELU KATA YA BUSWELU, WILAYA YA ILEMELA AKITOKEA ENEO LA IGOMBE KWAKUTUMIA USAFIRI WA PIKIPIKI YENYE USAJILI MC 742 CKK AINA YA SANYA AKIWA NA GUNIA 3 ZA BHANGI. AMBAPO BAADA YA MAHOJIANO MTUHUMIWA AMEFANIKISHA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA MWINGINE ALIYEKUWA ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI AKIWA NA GUNIA 3 ZA BHANGI. UPELELEZI UNAKAMILISHWA NA WOTE WATAFIKISHWA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO.
TUKIO LA NNE
WATUHUMIWA WA KESI MBALIMBALI WALIOFIKISWA MAHAKAMA MBALIMBALI ZA MKOA WA MWANZA NA JESHI LA POLISI WAMEPATIKANA NA HATIA NA KUHUKUMIWA KULINGANA NA MAKOSA YAO KAMA IFUATAVYO:-
WILAYA YA ILEMELA
KOSA 1: KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA (BHANGI)
MTUHUMIWA, EMMANUEL SWEETBERT AMEHUKUMIWA JELA MIAKA 30.
KOSA2: KUMPA MIMBA MWANAFUNZI
MTUHUMIWA, JAPHET MUSIBA AMEHUKUMIWA JELA MIAKA 30.
MTUHUMIWA, SAMWEL MAJALA AMEHUKUMIWA JELA MIAKA 30.
KOSA3: KUFANAYA MAPENZI NA MWANAFUNZI
MTUHUMIWA, DAUD ELIAS AMEHUKUMIWA JELA MIAKA 30.
KOSA3: KULAWITI
MTUHUMIWA, MAUNDA MASATO AMAHUKUMIWA JELA KIFUNGO CHA MAISHA.
KUELEKEA IBADA ZA PASAKA
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VINGINE VYA USALAMA LIMEJIPANGA VYEMA KUHAKIKISHA IBADA ZA PASAKA KUANZIA IJUMAA KUU MPAKA JUMATATU YA PASAKA ZINAKUWA KATIKA MAZINGIRA YA USALAMA.
DORIA ZA MIGUU, PIKIPIKI NA MAGARI KATIKA MAENEO YOTE ZITAIMARISHWA, PIA MAENEO YA MAJINI NA VISIWA VYOTE PATAKUWA SALAMA. JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWATAKA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA KUFICHUA VITENDO VYA UHALIFU NA WAHALIFU ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA.
Post a Comment